Tuesday, October 27, 2020

SIMBA WATAJWA KIPIGO CHA NDANDA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI


KIPIGO cha mabao 4-0 walichopata Ndanda katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kutoka kwa Yanga kimetajwa kuchangiwa na matokeo ya Simba.

Yanga ambao walitoka sare ya kufungana bao 1-1 na African Lyon kabla ya kukutana na Ndanda, walihitaji ushindi wa hali na mali ili waweze kufukuzana na Simba kileleni.

Akizungumza na BINGWA juzi, kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema ilikuwa lazima washinde kwa Ndanda ili waweze kumkaribia mpinzani wao Simba.

Mwambusi alisema walihitaji kupata pointi tatu kwa lengo la kutaka kutetea ubingwa wao, lakini kutoachwa mbali na  Simba waliokuwa wanaongoza kwa pointi 41 kabla ya mchezo wao wa jana dhidi ya Ruvu Shooting.

Alisema sababu nyingine ya kuipa dozi kubwa inatokana na Ndanda ni moja ya timu ambazo zinawasumbua kupata matokeo mazuri, kwani katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, walitoka sare tasa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

“Mchezo ulikuwa ngumu lakini tulihitaji pointi tatu na tunashukuru tumezipata, tulitaka kumkaribia mpinzani wetu na kujiwekea mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wetu,” alisema Mwambusi.

Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Ndanda, Hamimu Mawazo, amesema sababu ya timu yake kupoteza michezo mitatu mfululizo ya mzunguko wa pili inatokana na kubadilisha makocha kila kukicha.

Mawazo alisema tatizo la kubadilisha makocha limekuwa sugu kwani wachezaji wanashindwa kuzoea mfumo wa kocha mmoja.

Alisema timu hiyo inahitaji kukaa na kocha mmoja kwa muda ili kuzoea mfumo wake.

“Matokeo ya leo (juzi) hayajanifurahisha lakini nahitaji muda kuijenga timu kwani nimeichukua si muda mrefu tangu kocha wetu aondoke na kubadili makocha katikati ya msimu ni hatari,” alisema Mawazo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -