Wednesday, October 28, 2020

SIMBA WATEKA VIJIJI WAKIELEKEA MTWARA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU, MTWARA

KIKOSI cha Simba kimeteka baadhi ya vijiji kikielekea mkoani Mtwara kwa mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda, utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Wekundu hao wa Msimbazi waliondoka jana jijini Dar es Salaam, wakiwa na kikosi chote kilichosajili wakiwamo wachezaji wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo lililotarajia kufungwa usiku wa kuamkia leo.

Kikosi hicho cha Simba kilionekana kulakiwa na mashabiki wao wengi walipokuwa wakipita katika vijiji vya mkoa huo huku wakitaka kuona baadhi ya wachezaji wapya waliosajili katika kipindi hiki.

Hata hivyo, Simba wameondoka huku kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog, akiwa na matumaini makubwa ya kushinda kutokana na maandalizi kabambe aliyoyafanya kabla ya kukutana na wenyeji, Ndanda.

Omog alisema amefanikiwa kukiandaa kikosi kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha wanarejea jijini Dar es Salaam na pointi tatu ambazo zitawawezesha kuendelea kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo.

Alisema kwa kiasi kikubwa ametengeneza kikosi bora ambacho kitaleta ushindani na kupata mafanikio wakianzia mchezo huo ambao ni muhimu kushinda.

Omog alisema amewaandaa wachezaji wake kisaikolojia, lakini pia kucheza katika viwanja vibovu ili kukabiliana na mazingira yote kuhakikisha wapata ushindi.

“Tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi katika viwanja vya mikoani ambavyo miundombinu yake inafanana,” alisema Omog.

Kikosi kilichoondoka jana ni Daniel Agyei, Mohamed Hussein, Abdi Banda, Muzamir Yassin, Jonas Mkude, Ibrahim  Ajib, James Kotei, Laudit Mavugo, Fredrick Blagnon na Manyika Peter.

Wengine ni Denis Richard, Jamal Mnyate, Said Ndemla, Shiza Ramadhan ‘Kichuya’, Juma Luizio, Javier Bokungu, Novaty Lufunga, Method Mwanjale na Mohamed Ibrahim.

Wachezaji ambao hawajaambatana na kikosi hicho ni Mwinyi Kazimoto, Peter Semwanza, Pastroy Athanas huku Vincent Angban na Mussa Ndusha wakitajwa kutemwa katika usajili wa timu hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -