Monday, November 30, 2020

SIMBA WAWAPIGA PINI AJIBU, MKUDE NA BANDA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY,

HUKU wakiwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wameonyesha kutokuwa na mzaha na kikosi chao baada ya kuanza mchakato wa kuwaongezea mkataba wachezaji wao nyota, wakiwamo wale wanaotajwa kuwaniwa na watani wao wa jadi, Yanga.

Wachezaji nyota wa Simba wanaotolewa macho na Yanga ni pamoja na Ibrahim Ajib, Jonas Mkude na Abdi Banda.

Wakati Ajib akionekana kama pacha sahihi wa mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, Mkude ndiye anayetajwa na klabu hiyo ya Jangwani kama mtu sahihi wa kutatua tatizo sugu linalowakabili la kiungo mkabaji kama ilivyo kwa kiraka Banda.

Katika safu ya kiungo mkabaji, Yanga wamekuwa wakimtumia Mzambia Justin Zulu ambaye hata hivyo ameshindwa kuonyesha kile kilichokuwa kikitarajiwa na mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Bara kama ilivyo kwa nyota wa Zanzibar, Said Juma Makapu.

Kutokana na hali hiyo, Yanga imeona ni vema ikatupia macho kwingineko kupata mchezaji wa kuziba nafasi hiyo ambapo mara zote, wamekuwa wakiangukia kwa Mkude ambaye ameonyesha kuwa ni mmoja wa viungo bora kabisa hapa nchini.

Kwa kufahamu hilo, Simba wameonekana kushtukia mchezo na hivyo kuamua kumalizana fasta na nyota wao wote muhimu ili kuwakata maini Yanga.

Taarifa ambazo BINGWA limezipata zinadai kuwa, mkataba walioingia Ajibu na Mkude ni wa miaka miwili, lakini umeboreshwa baadhi ya vipengele ikiwemo kuwaruhusu iwapo itatokea timu inawahitaji nje ya Tanzania.

Akizungumza na Bingwa, Mkude alisema sasa hivi tayari ana mkataba na Simba ambao utambakisha kwa kipindi kingine.

“Nina mkataba na Simba wa muda mrefu, hivyo siwezi kuyazungumzia tena masuala hayo kwani nina kazi kubwa ya kuisaidia timu yangu iweze kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema.

Naye Ajib alisema: “Sipendi kuzungumzia masuala ya mkataba wangu na sijui nani amezieneza hizi taarifa,  naomba ieleweke nina mkataba na Simba ingawa siwezi kusema unamalizika lini.”

Kwa upande wa Banda, aligoma kuongeza mkataba mpya hadi pale atakapoboreshewa mshahara, makazi pamoja na mkataba kuwa na mwaka mmoja usiombana iwapo kama atapata timu nje, kitu ambacho ni kinyume na ule wanaotaka kumpa Simba wa miaka miwili.

Mbali na hiyo, Banda amepata ofa mbili kutoka Afrika Kusini ambapo atajiunga na timu hizo watakapokuwa wamekwishafikia makubaliano.

Kwa sasa Simba wapo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 55, baada ya michezo 24 waliocheza, wakifuatiwa na mahasimu wao Yanga wenye pointi 53.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -