Wednesday, October 21, 2020

SIMBA YAANZA USAJILI UJAO MAPEMA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA SAADA SALIM

SIMBA hawataki kurudi walikotoka tena baada ya miaka kadhaa ya mateso ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa, hivyo wameamua kuanza mapema harakati za usajili wa msimu ujao.

Msimu huu Wekundu hao wameonekana kupatia baada ya kusajili wachezaji kadhaa wanaoonekana kuleta tija kwenye klabu hiyo ambapo wameiwezesha kukamata usukani wa ligi.

Nyota wapya waliotua Simba msimu huu na wanaoonekana kutoa mchango wa maana ni pamoja na winga Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim na Pastory Athanas.

Habari za ndani zilizonaswa na gazeti hili zinadai kuwa uongozi wa klabu hiyo tayari umeanza kufanya ‘skauti’ kwa ajili ya usajili wa msimu ujao.

Imeelezwa kuwa ili kuhakikisha inasajili wachezaji makini badala ya kubahatisha, maskauti wa klabu hiyo watafuatilia michezo mbali mbali ya ligi kuu msimu huu ili kubaini wachezaji wakali ambao wanaweza kutua Msimbazi.

“Tayari maskauti wameanza mzunguko wa pili, mikakati hiyo imetokana na Pastory pamoja na Kichuya kuonyesha kiwango kizuri, tunaamini badala ya kupoteza fedha nyingi kwa ajili ya kutafuta wachezaji nje ya nchi tunaweza kuwapata hapa hapa nchini na wakatusaidia,” alisema mmoja wa mabosi wa Simba.

“Licha ya kwamba lengo ni kupata wachezaji makini, lengo jingine ni kupunguza gharama za usajili ambazo tumekuwa tukikutana nazo kwa wachezaji wa kigeni.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -