Saturday, November 28, 2020

Simba yafanya kufuru kwa Tshabalala

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ASHA MUHAJI

SIMBA imefanya kufuru baada ya kumpa mkataba mnono wenye thamini ya Sh milioni 60, beki wake wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, ili kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Tshabalala, aliyesajiliwa na klabu hiyo katika misimu mitatu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, akitokea Kagera Sugar, anatarajia kusaini mkataba huo mpya kesho.

Katika mkataba wake wa awali uliodumu kwa miaka mitatu, ulikuwa wa thamani ya Sh milioni 12,000, sawa na ongezeko la Sh milioni 48,000 katika mkataba mpya wa miaka miwili utakaomalizika 2019.

Akizungumza na BINGWA jana, Meneja wa mchezaji huyo, Heri Mzozo, alisema masuala yote ya msingi kati ya pande hizo mbili yamemaliza kwa asilimia 80, hivyo kusubiri kutia saini mkataba mpya.

Mzozo alisema kabla ya kufikia dau hilo, Simba walikuwa wametoa ofa ya Sh milioni 40, lakini kwa upande wao, walisimamia dau la Sh milioni 60, ikiambatana na marupurupu kadhaa ambayo alikataa kuyaweka wazi kwa sasa.

Alisema akiwa ni meneja wa mchezaji huyo, ameamua kumbakisha Simba kutokana na umri wake kuwa bado mdogo, ili aendelee kukuza kipaji chake ndani ya klabu hiyo, ambayo imeonekana dhahiri kama nyota yake iko huko.

“Kwakweli ndani ya mkataba huu hakukuwa na matatizo, japo inawezekana kama binadamu wakatofautiana kidogo, isipokuwa msingi unabaki palepale kuwa alikuwa na maisha mazuri ndani ya timu hiyo na mimi sijaona sababu ya kumhangaisha mchezaji, tamaa pia si nzuri, ni vema ukaheshimu utu,” alisema.

Akizungumzia sababu za kuingia mapema mkataba mpya ilhali ule wa zamani unamalizika Juni 2017, Mzozo aliweka wazi ni kutaka kumaliza usumbufu ambao wamekuwa wakiupata kutoka kwa timu nyingine zikitaka kumweka sawa ili muda ukifika atie saini katika moja ya klabu hizo.

“Timu nyingi zilishaanza usumbufu, nami nafahamu wazi sheria, hatukuruhusiwa kufanya mazungumzo na timu yoyote kwa vile muda huo ilikuwa bado, hivyo ili kukata mzizi wa fitina, nimeona bora tumalizane na mwajiri wake wa sasa, kwani hata kijana bado anafurahia maisha ndani ya klabu hiyo.

“Ipo mifano ya wengi waliopotea stepu, hivyo sikutaka mchezaji wangu naye aje apotee kutokana na kuchanganywa  katika vishawishi vinavyoweza kumfanya asicheze mpira.  Tshabalala bado mdogo, ana uwezo, pia umri unamruhusu kucheza muda mrefu, hivyo ninataka atimize ndoto zake,” alisema.

Kusaini mkataba kwa mchezaji huyo kutamaliza hofu iliyoanza kutawala miongoni mwa mashabiki wa timu hiyo, kama huenda angetimka na kuiacha kwenye mataa timu yake ambayo hivi sasa inapambana kutwaa ubingwa ilioukosa kwa misimu mitatu sasa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -