Tuesday, December 1, 2020

SIMBA YAISHTUKIA YANGA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA SAADA SALIM

SIMBA imeshtukia janja ya Yanga ya kutaka kuwahujumu kwenye michezo yao miwili ya Kanda ya Ziwa, dhidi ya Mbao na Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza na hivyo kujizatiti kuwakata maini watani wao hao wa jadi.

Baada ya Simba kupoteza mechi yao dhidi ya Kagera Sugar wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba kwa kufungwa mabao 2-1, kitendo hicho kilikuwa ni faida kwa Yanga kuelekea kampeni yao ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa sasa wakiwa kileleni mwa ligi kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Simba, Yanga wameonekana kujipanga upya kuona ni vipi wanazidi kuwamaliza watani wao hao walioshikilia usukani wa ligi kwa muda mrefu ili mwisho wa siku, waweze kulibakiza kombe Jangwani.

Kwa kulifahamu hilo, Simba wameamua kuja kivingine kwa kuhakikisha hawatoi mwanya kwa mtu yeyote kupenyeza mkono kwenye mechi zao, lakini pia kuhakikisha kila mchezaji wao anawajibika kadri ya uwezo na nafasi yake.

Taarifa za uhakika zilizoifikia BINGWA jana, zinasema kwamba kuna baadhi ya mashabiki wanaodaiwa kuwa wa Yanga wanaojifanya ni Wanamsimbazi ambao wamekwenda eneo la Busisi kuwapokea wachezaji wa Simba wanaotokea Geita ili kujichanganya nao na kupenyeza ‘sumu’.

Baadhi ya mashabiki wa Tawi la Mpira Pesa ambao wako mkoani Geita, wametamba kuwadhibiti ‘mamluki’ hao ili kupangua njama za hujuma dhidi ya kikosi chao.

Mmoja wa mashabiki hao ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini kwa madai kuwa si msemaji wa tawi lao, alisema: “Tumetahadharishwa kuwa kuna watu wa Yanga wamepanga kujipenyeza kwenye msafara wetu wakijifanya ni wenzetu, tunawaambia wasithubutu kufanya hivyo, kwani tutawaumbua, hatutakuwa tayari kufanya makosa kwa mara nyingine.”

Juu ya hali ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao, Meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan `Mgosi`, ameliambia BINGWA kuwa, wanaendelea vema na maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Mbao FC keshokutwa kabla ya kuivaa Toto African.

“Kufungwa (dhidi ya Kagera Sugar) si kitu kizuri, lakini haina maana kwamba suala hilo limetuchanganya, vijana wako vizuri tayari kwa mchezo ujao na kurekebisha makosa yaliyoonekana katika mechi iliyopita,” alisema.

Mgosi alisema mchezo ujao utakuwa muhimu zaidi ya mchezo wa awali na kwamba wanataka kufanya vizuri, hilo likiwa ni azimio la wachezaji wao pamoja na benchi la ufundi.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba wako nafasi ya pili wakiwa na pointi 55, huku Yanga wakiongoza kwa pointi 56, wakati Kagera Sugar ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 45, wakiwatupa Azam nafasi ya nne kwa tofauti ya pointi moja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -