Saturday, January 16, 2021

SIMBA YAITANGAZIA KIAMA MBAO FC

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MASYENENE DAMIAN, MWANZA

SIMBA wameitangazia kiama Mbao FC baada ya kusema wataibuka na ushindi mnono katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.

Tayari Simba wamewasili jijini hapa, ambapo jana asubuhi walifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja huo kujiandaa na mchezo huo.

Akizungumzia matayarisho ya mchezo huo, Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, Iddi Kajuna, alisema kikosi chao kipo kamili kwa kuendekeza ushindi.

Kajuna alisema wachezaji waliokuwa majeruhi akiwamo mshambuliaji wao, Juma Luizio, wamerejea mazoezini na Mbao FC wajiandae kupokea kichapo.

“Tumekuja tukiwa kamili, ni mchezaji mmoja tu ambaye atakosekana kwa sababu ya matatizo ya kifamilia.

Mechi zote kwetu tunazipa umuhimu sawa, lakini hatujawahi kuiogopa timu  na hatuiogopi Mbao FC, msimu uliopita  tuliwafunga mechi zote mbili na ile ya mashindano ya Kombe la Shirikisho,” alisema Kajuna.

Alisema malengo yao ni kushinda si chini ya mabao matatu ili waweze kujiweka katika mazingira bora ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.

“Plan (mkakati) yetu ni kupata mabao ya mapema katika mchezo wa kesho na falsafa yetu kwa sasa ni kupata ushindi wa kuanzia mabao 3 na zaidi, haijalishi timu gani tunakutana nayo,”

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Jackson Mayanja, alisema maandalizi yako vizuri na wachezaji wana morali ya hali ya juu katika kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Mayanja alisema kutokana na maandalizi yaliyofanywa, ana imani yatakuwa na faida kwao kwa kuwa msimu huu ana wachezaji wenye uzoefu mkubwa.

“Usajili tulioufanya ni kutokana na mapungufu ya msimu uliopita, kwa hiyo msimu huu tunategemea tu ushindi mnono na si vingine.

Alisema katika kikosi chao kuna wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza soka na na si kweli kwamba wanamtegemea  Emmanuel Okwi, aliyefunga mabao sita katika mechi mbili alizocheza.

Kwa upande wake, John Bocco ambaye ni mshambuliaji wa timu hiyo, alisema wamemaliza mazoezi yao salama na wanawaheshimu Mbao FC.

Bocco alisema kwa maandalizi waliyofanya ana imani wataibuka na pointi tatu katika mchezo huo wa leo utakaopigwa kuanzia saa 10 jioni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -