Wednesday, November 25, 2020

SIMBA YAITESA YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

YANGA wanajua wana kibarua kigumu cha kutetea ubingwa wao kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, sasa wanasaka ushindi kwa nguvu zote ili waweze kuwaengua kileleni watani wao wa jadi, Simba.

Kutokana na kutambua hilo, Yanga wameanza kuweka mkakati na mbinu zitakazowawezesha kushinda mchezo wa marudiano wa ligi hiyo dhidi ya Azam, utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga wanaona mchezo huo ni muhimu kwa kushinda na wakipoteza watakuwa wameongeza pengo la pointi na kuwa kubwa ikiwa Simba wataifunga Kagera Sugar.

Simba, ambao wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 55, wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 53, wanatarajiwa kucheza Jumapili hii kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Pamoja na Yanga kukabiliwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya MC Alger, utakaochezwa Aprili 8 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini nguvu kubwa wameweka kwa mchezo wao dhidi ya Azam.

Viongozi wa matawi ya Yanga jana waliitisha kikao kizito kilichofanyika katika makao makuu ya klabu hiyo kwa lengo la kujenga mikakati itakayofanikisha ushindi, ikizingatia walifungwa mabao 4-0 na Azam kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyofanyika Januari, mwaka huu.

Kikao hicho kilifanyika kwa siri, kwani viongozi wa matawi hayo hawakutaka taarifa ya kikao iandikwe kwenye magazeti ili kuepuka hujuma.

Mmoja wa viongozi wa matawi hayo, alisema waliitisha kikao hicho kwa lengo la kupanga mikakati itakayosaidia kushinda katika mechi mbili dhidi ya Azam na Waarabu hao wa Algeria.

Alisema katika kikao hicho walifanikiwa kuunda kamati mbalimbali ambazo zitashughulika na fitina, ulinzi na usalama na kamati ya kuhamasisha ushindi.

Kiongozi huyo alisema kamati hizo zitakuwa na kazi moja ya kuhakikisha zinapambana na kuziba mianya ya aina yote ya hujuma ndani na nje ya uwanja.

“Dhamira ya kikao ni kuhakikisha tunashinda michezo yetu yote inayotukabili, hivyo tupo hapa tunajadiliana ni vipi tutaandaa silaha za maangamizi,” alisema.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alithibitisha kuwapo kwa kikao cha viongozi wa matawi ya klabu hiyo.

“Ni kweli kuna kikao cha kupanga mikakati mbalimbali, unajua ligi inaelekea ukingoni, sasa lazima mambo yakae sawa, lakini kilichozungumzwa tutawafahamisha muda ukifika,” alisema.

Mkwasa alisema kuwa, kikosi hicho kinaendelea na maandalizi ya nguvu ili kuweza kupata matokeo mazuri kwenye mechi hizo zinazokuja.

Wachezaji wa timu hiyo wanaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -