Wednesday, November 25, 2020

SIMBA YAIWEKA ROHO JUU KAGERA SUGAR

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MARY PETER,

SIMBA imeiweka roho juu Kagera Sugar, baada ya uongozi wa klabu hiyo kuanza kuwahofia waamuzi watakaochezesha mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa Aprili 2 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Akizungumza na BINGWA jana, mratibu wa timu hiyo, Mohamed Hussein, alisema wanahitaji kuona waamuzi wanazingatia sheria 17 za soka ili mshindi apatikane kutokana na uwezo wake.

Hussein alisema mchezo huo ni muhimu kushinda baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho (FA) kwa kufungwa mabao 2-1 na Mbao kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Alisema ushindi kwao utawawezesha kufikisha pointi 45 katika msimamo wa ligi hiyo ambapo Simba wanaongoza kwa pointi 55.

Hussein alisema ana imani mchezo huo ukichezeshwa kwa kuzingatia sheria za soka timu itakayoibuka na ushindi itatokana na maandalizi waliyofanya.

“Mara nyingi waamuzi wa Tanzania huingia na matokeo uwanjani hasa pale timu ndogo zinapokutana na timu kubwa ikiwamo Simba na Yanga.

Kama mwamuzi atatumia vyema filimbi yake nina imani kubwa Simba hawatatoka na pointi katika Uwanja wa Kaitaba,” alisema.

Hussein alisema watahakikisha wanatia doa harakati za mbio za ubingwa Simba kwa kuifunga katika mchezo huo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -