Friday, September 25, 2020

Simba yaja kivingine

Must Read

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi...

NA ASHA KIGUNDULA

KAMA kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa, basi Simba hii itakuwa moto wa kuotea mbali, hasa linapokuja suala la gharama za uendeshaji wa klabu.

Iko hivi, uongozi wa klabu ya Simba umekuja na mkakati mpya, ukiwataka wanachama wa klabu hiyo kuchangia klabu yao kwa kutumia  kadi za kiektroniki.

Kwa hesabu zilizopo, klabu hiyo itakuwa na uhakika wa kukusanya shilingi bilioni 65 kwa mwaka, kiasi ambacho kitaifanya  kuwa levo nyingine kama ilivyo TP Mazembe  ya DR Congo au Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema katika Mkoa wa Dar es Salaam,  tayari baadhi ya mashabiki wameanza kujiunga kwa kuchukua kadi hizo, ambazo zitaongeza pato la klabu yao.

Manara alisema gharama ya kadi hiyo ni shilingi 22,000, huku shilingi 14,500 ikielekezwa moja kwa moja kwenye mfuko wa klabu.

Alisema kukuza pato la klabu yao kutawapa uwanja mpana wa kuiendesha kisasa, ikiwamo kusajili wachezaji wa viwango vya juu, ambao hugharimu fedha nyingi.

“Wapenzi wa klabu ya Simba Tanzania nzima, mjitojkeze kujiunga.  Ni kama ilivyo Uingereza. Mimi ni mmoja wa mashabiki wanaochangia klabu yangu kwa kutoa ada ya uanachama kwa mwaka.

“Sasa ni zamu yenu katika klabu yenu ya Simba. Mjiunge ili klabu izidi kwenda kisasa zaidi,” alisema Manara.

Aliongeza kuwa hii ni mara ya pili kwani walizindua mpango huo,  Desemba 14, mwaka jana, kwa kufungua rasmi kupitia Benki ya Equity, ambapo awamu ya pili imeanza kupitia matawi ya benki hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Moshi, Morogoro, Arusha, Mbeya na Zanzibar.

Katika hatua nyingine, Manara alidokeza kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, atazindua kadi za kielotroniki kwa mashabiki Januari 29, mwaka huu, bungeni jijini Dodoma.

Alisema baada ya Spika Ndugai kuzindua kadi hizo, naye atakabidhiwa ya kwake kwa kuwa ni shabiki na mwanachama wa Simba, pamoja na wabunge wengine.

“… Lengo letu, tunaka ndani ya mwaka huu tuwe tumeuza kadi 100,000 kwa mashabiki,” alisema Manara, akiongeza kuwa shabiki atalazimika kuwa na kitambulisho cha Taifa au kile cha kura, ambacho ataambatanisha na barua ya Serikali ya mtaa.

Wakati huo huo, Manara alisema mchezo wao wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa kesho dhidi ya Mwadui umehamishiwa Uwanja wa Taifa, badala ya Uhuru.

Alisema wanashukuru ombi lao la kutaka mchezo huo uchezwe Uwanja wa Taifa limekubaliwa, hivyo amshabki wajitokeze kushuhudia burudani itakayoanza saa 10 jioni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi tatu kila mchezo, wakianzia mechi...

CHAMA GUMZO KILA KONA

NA WINFRIDA MTOI KIWANGO kilichoonyeshwa na kiungo wa Simba, Clatous Chama katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania...

United ‘kimeo’ yamtoa povu Evra

MANCHESTER, EnglandBEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili.
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -