Friday, December 4, 2020

Simba yajibu mapigo Yanga

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

WINFRIDA MTOI NA SALMA MPELI,

BAADA ya Shiza Kichuya kuongoza kwenye orodha ya wafungaji na kwenye klabu yake ya Simba kuonekana kuwa ni tegemeo namba moja, kuliibuka maneno mengi kutoka kwa mashabiki wa Yanga wakidai watani wao wanamtegemea mchezaji huyo pekee kwenye suala zima la ufungaji.

Katika kuwadhihirishia watani wao kuwa wanachokisema hakina mashiko, ni kuwajibu kwa vitendo kwenye michezo miwili ya mwisho kikosi cha Simba kilipoibuka na ushindi huku wafungaji wa mabao yake wakiwa ni wachezaji wengine tofauti na Kichuya.

Licha ya mchezaji huyo ambaye kwa sasa nyota yake inang’aa zaidi kwenye kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi kushindwa kufunga bao kwenye michezo hiyo ya mwisho, lakini Simba iliendelea kuibuka na ushindi wa kishindo kama kawaida yao.

Kichuya hakuweza kufunga kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC, wakati Simba ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mzamiru Yassin, lakini pia katika mechi ya Jumapili dhidi ya Toto Africans ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku Kichuya akitoka bila kufunga.

Mabao hayo yaliyofungwa na mshambuliaji huyo raia wa Burundi, Laudit Mavugo na Mzamiru aliyetupia mabao mawili hivyo kuwa jibu tosha kwa wapinzani wao wa jadi kwamba  wana kikosi kipana cha kuzalisha mabao bila ya kumtegemea Kichuya pekee.

Kutokana na hali hiyo, Simba imeongeza idadi ya wafungaji kati ya wale wanaoongoza kwa ufungaji kwenye orodha ya wafungaji ambapo Mzamiru amefikisha mabao manne, Mavugo na Ibrahim Ajib, wakiwa na matatu kila mmoja huku Kichuya akiendelea kuongoza akiwa na mabao saba.

Aidha, uwezo alioonyesha, Mohammed Ibrahim, juzi aliweza kucheza dakika zote 90 za mchezo tofauti na awali alipokuwa anatokea benchi na kwenda kubadilisha mchezo.

Yanga wanajivunia washambuliaji wao, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Obrey Chirwa, wote wakiwa na mabao manne kila mmoja ambayo yameshafikiwa na Mavugo na Mzamiru.

Simba imeendelea kuota mizizi kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiongoza na pointi 29 na michezo 11 waliyocheza, ambapo kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuondoka kesho kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Stand United na Mwadui FC.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -