Friday, November 27, 2020

SIMBA YAKABIDHI WACHINJAJI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ZAINAB IDDY NA WINFRIDA MTOI

WASHAMBULIAJI wa Simba, Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo, ndio wanaotegemewa kupachika mabao,  baada ya kuandaliwa kuanzishwa pamoja katika mchezo wa marudiano  wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara.

Katika mazoezi yao ya mwisho yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam, kocha wa timu hiyo, Joseph Omog, alionekana kutumia muda kuwaandaa wachezaji hao na inavyoonekana wataanzishwa katika mchezo wao dhidi ya Ndanda.

Omog alionekana kuwafua vilivyo washambuliaji hao huku akiwapa mbinu tofauti za kuhakikisha hawafanyi makosa wanapokuwa karibu na eneo la hatari, lakini hata nje ya 18.

 

Kutokana na Omog kujua mazingira ya Uwanja wa Nangwanda Sijaona, alionekana kuwapa mbinu tofauti wachezaji wake jinsi ya kukabiliana na mazingira ya uwanja huo kwa kuwataka kupiga mashuti ya mbali.

Kocha huyo alionekana kumpa majukumu makubwa Kichuya ya kuhakikisha anatumia ipasavyo mipira inayokufa, lakini kupiga vizuri mipira ya kona itakayozaa matunda.

Lakini Kichuya akishindwa kufunga  mipira ya moja kwa moja ya kona, Ajib na Mavugo wawe tayari kutingisha vyavu za wapinzani wao.

Hata hivyo, Omog alionekana kutumia muda mwingi kuwaandaa wachezaji akiwamo Mwinyi Kazimoto na Abdi Banda kupiga kwa ufasaha mipira ya faulo ili kuhakikisha wanafunga.

Katika mazoezi hayo waliyotumia saa moja na nusu, kocha huyo wa Simba pia alikuwa na jukumu la kuwafua mabeki wake wa pembeni, Mohamed Hussein na Javier Bokungu, kuhakikisha muda wote wanakuwa makini na kutoruhusu kupitwa na mshambuliaji, lakini kuanzisha mashambulizi pale inapoonekana washambuliaji wake kuzidiwa ujanja na wapinzani wao.

Katika hatua nyingine, kocha wa makipa wa timu hiyo Mkenya, Idd Salimu, alionekana kumwaandaa Manyika Peter, kudaka baada ya Vincent Angban kutemwa katika kikosi hicho.

Angban ambaye alidaka katika mzunguko wote wa kwanza wa ligi hiyo, amejikuta akitemwa baada ya kuonyesha udhaifu mkubwa katika mechi mbili za mwisho kwa kuruhusu mabao matatu.

Kipa huyo alitibua rekodi ya Simba ambao walikuwa hawajafungwa hadi mzunguko wa 13 pale alipofungwa bao 1-0 na African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kabla ya kupoteza kwa Tanzania Prisons baada ya kupigwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -