Tuesday, November 24, 2020

SIMBA YAKAMILISHA SAFU YA UBINGWA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

KIKOSI cha Simba cha ubingwa kimekamilika baada ya mabeki wake wa kutumainiwa, Method Mwanjali na Jjuuko Murshid, kurejea uwanjani huku wakitarajiwa kuanza kazi kwa kuivaa Madini katika mchezo wa robo fainali wa Kombe la Shirikisho (FA).

Mwanjali ameanza mazoezi makali baada ya kushindwa kucheza michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la FA kutokana na kuwa majeruhi huku Jjuuko akiwa hajakichezea kikosi hicho tangu alipokuwa na timu yake ya Taifa ya Uganda kwenye michuano ya Kombe la Afrika (Afcon) iliyomalizika mwezi uliopita nchini Gabon.

Wawili hao wanatarajia kuunda kombinesheni kali baada ya kutokuwa pamoja kwa muda mrefu tangu michuano ya Afcon ilipoanza Januari 14, mwaka huu.

Akizungumza na BINGWA, Mratibu wa Simba, Abasi Ali, alisema Mwanjali ameanza mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam kujiandaa na michezo ya ligi na Kombe la FA.

“Mwanjali amefanya mazoezi toka juzi kabla ya kujumuishwa na wenzake katika kikosi kitakachoanza dhidi ya Madini,” alisema.

Alisema Jjuuko naye kwa sasa yuko fiti kuitumikia Simba katika mechi mbalimbali na kwamba sasa kikosi chao kimekamilika kwa ajili ya kumalizia hatua iliyobaki ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA msimu huu.

“Naweza kusema kwamba kikosi cha ubingwa kimekamilika, sasa hatuna hofu na ukuta tena maana majembe mawili yameimarika, timu iko vizuri na kurejea kwa wachezaji hawa maana yeke safu yetu ya kutupa taji msimu huu imekamilika,” alisema.

Katika hatua nyingine, Abasi alisema wachezaji wao wanatarajia kuondoka leo kwenda Dodoma kwa mwaliko maalumu kutoka kwa Chama cha Soka mkoani humo (Dorefa).

Abasi alisema wakiwa mkoani humo watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -