Saturday, November 28, 2020

SIMBA YAKWAMA KAITABA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU, KAGERA

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba, jana walishindwa kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, baada ya kutandikwa mabao 2-1 na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.

Matokeo hayo ni machungu sana kwa Simba ambayo sasa imeendelea kubaki katika nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 55, nyuma ya mahasimu wao Yanga ambao wanaongoza ligi hiyo kwa pointi 56, baada ya juzi kuilaza Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa ni wa marudiano wa mzunguko wa pili, baada ya mechi ya mzunguko wa kwanza Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu na kutokea kosakosa za hapa na pale.

Dakika ya 11 Seleman Mangoma alijaribu kutaka kuifungia Kagera bao la kuongoza baada ya mabeki wa Simba kufanya makosa, lakini kipa Daniel Agyei aliokoa shuti lake.

Kama safu ya umaliziaji ya Simba ingekuwa makini, basi wangeweza kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kwani walipata nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba, Laudit Mavugo, kiungo mahiri Said Ndemla, walishindwa kusimama vema mbele na kujikuta wakikosa mabao ya wazi mara kwa mara timu hiyo iliposhambulia.

Kagera Sugar ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 27, kwa bao safi lililofungwa na mshambuliaji wake hatari, Mbaraka Yusuph ambaye aliachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja kimiani.

Ibrahimu Ajibu nusura aipatia Simba bao la kusawazisha katika dakika ya 40 ya mchezo huo baada ya kupiga mkwaju wa adhabu kwa shuti kali lakini lililokwenda nje.

Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika na kwenda mapumziko, Simba tayari walikuwa nyuma kwa bao moja.

Kagera walikianza kipindi cha pili kwa kasi kubwa na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa dakika ya 46 na mshambuliaji wake, Edward Christopher, akipokea pasi ndefu ya Seleman Mangoma na kumtungua kipa wa Simba Agyei.

Licha ya kuwa nyuma kwa mabao mawili, Simba hawakukata tamaa na hivyo kuendelea kupambana na hata dakika ya 61 waliweza kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Mzamiru Yasini, baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la Kagera na hivyo kufanya matokeo kuwa 2-1.

Katika michezo mingine ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa jana, Afrika Lyon waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Shukrani pekee ni kwa mfungaji wa bao hilo, Abdallah Mguhi, katika dakika ya 42 ya mchezo huo ambalo lilidumu hadi mwisho mwa mchezo.

Katika Uwanja wa Majimaji Songea, wenyeji Majimaji waliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza, mabao yao yalifungwa na Kelvin Sabato, Peter Mapunda, Masele Boniventure na George Mpole.

Kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, wenyeji Mwadui walilazimishwa  sare ya mabao 2-2 na JKT Ruvu, huko Mbeya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -