Friday, October 30, 2020

SIMBA YAMZUIA AJIB

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SAADA SALIM

BAADA ya Simba kuporwa mshambuliaji, Ibrahim Ajib na mahasimu wao Yanga, klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi imeamua kuja na mpango kabambe wa kuhakikisha nyota huyo hatambi mbele yao.

Klabu hiyo ambayo sasa iko chini ya Salim Abdallah ‘Try Again’ ambaye anakaimu nafasi ya Rais Evance Aveva na nafasi ya Makamu Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ikichukuliwa na Idd Kajuna, baada ya wawili hao kufunguliwa mashtaka ya utakatishaji fedha, imeendelea na mikakati yao kuendeleza klabu hiyo mojawapo ikiwa ni ‘kumpiga pini’ Ajib.

Katika kuhakikisha mapango wao wa kumdhibiti Ajib unatimia ili asije akaleta madhara kwao, uongozi wa klabu hiyo uko kwenye mchakato wa kumnasa beki wa kati wa Rayon Sport, Manzi Thierry.

Taarifa za kuaminika ambazo BINGWA ilizinasa jana kutoka kwa rafiki wa karibu wa mchezaji huyo wa Rwanda ni kwamba, kigogo mmoja wa Simba alikwenda nchini humo kufanya naye mazungumzo.

Alisema Simba imekuwa ikifanya mazungumzo na beki huyo ili kuafikiana kwa ajili ya kupata saini ya mchezaji huyo wa kutumainiwa wa Rayon.

“Ninachofahamu kwamba tayari Simba wanazungumza na Manzi, bila shaka kila kitu kinaenda vizuri na wakati wowote mchezaji huyo atajiunga na Wekundu wa Msimbazi,” alisema.

Rafiki huyo ambaye hakutaka kuandikwa jina lake, alisema kikubwa ambacho kinavutana kati ya Manzi ni kwamba Simba wanamtaka mchezaji huyo kufanya majaribio, kitu ambacho mwenyewe hakitaki.

“Suala la kufanya majaribio ndio limekuwa shida ila mazungumzo yanaendelea, wataafikiana na itakuwa msaada mkubwa sana kwa Simba kama watamalizana na mchezaji huyo,” alisema.

Pia Kamati ya Usajili ya Simba iko katika hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji kutoka Ghana, ambaye ujio wake utaambatana na kiraka wao, James Kotei anayewasili muda wowote kuanzia sasa kujiunga na kikosi hicho.

Simba wamekuwa wakifanya siri kubwa kuhusiana na mshambuliaji huyo hasa jina na timu anayotokea kwa hofu kuwa timu nyingine zinaweza kuwapiga bao na kumsajili.

Chanzo cha habari kimesema kwamba mazungumzo yanaendelea vizuri mara baada ya kiongozi, Abbas Ally aliyekwenda Ghana kwa kumalizana na mshambualiaji huyo, ambaye huenda akawasili hapa nchini hivi karibuni.

Alisema mazungumzo ya awali yamefanyika muda mrefu baada ya Abbas kwenda huku na kila kitu kimeenda vizuri na kusubiri siku ambayo atatua nchini kwa ajili ya kuingia naye mkataba wa makubaliano ya miaka miwili.
“Kwanza alianza kwenda mazoezi, alimuona na amechukua vipande vya video za baadhi ya mechi zake na pia mazoezini. Tayari watu wa kamati ya usajili na ufundi wanaonekana kumkubali,” kilisema chanzo hicho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -