Wednesday, August 12, 2020

Simba, Yanga safi ila msisahau jukumu kuu

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

MWANDISHI WETU

KWA wiki kadhaa sasa, klabu kongwe za Yanga na Simba zimegonga vichwa vya habari kuhusu matamasha yao maalumu ambayo yanaendana na kutambulisha wachezaji wapya waliowasajili. 

Jana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, umati mkubwa hususan wa mashabiki wa Yanga ulijitokeza kuadhimisha kilele cha Wiki ya Wananchi wakati Jumanne Agosti 6 mwaka huu katika uwanja huo huo, umati mwingine mkubwa safari hii wa mashabiki wa Simba unatarajiwa kujitokeza kuadhimisha kilele cha SportPesa Simba Week. 

Utamaduni huu ni wa kwanza kwa Yanga wakati Simba inaadhimisha miaka 10, na shukurani za kipekee ziende kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalili, na jopo lake la uongozi wakati huo kubuni wazo hilo. 

Sisi BINGWA tunawapongeza Simba na Yanga kwa kuandaa kitu kama hiki ambacho kina lengo la kuleta mashabiki karibu na timu yao. Moja ya vitu ambavyo vimenogesha matamasha haya mawili ni uuzaji wa jezi tena zile halisi (original). 

Kwa muda mrefu, wadau wamekuwa wakipigia kelele jinsi klabu hizi kongwe zinavyopoteza hela nyingi kwa jezi feki kuuzwa mitaani. Angalau safari hii tumeshuhudia klabu hizi zikizindua jezi zitakazotumika msimu ujao na vilevile kuwaelezea mashabiki wao ni sehemu gani wanaweza kupata. Aidha bei walizoweka kwa aina tofauti ya jezi watakazouza ni njia mojawapo ya kujiingizia mapato. 

Kilele cha tamasha la Wiki ya Wananchi ilikua mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya wakati hitimisho ya SportPesa Simba Week itakua mechi dhidi ya Power Dynamos ya Zambia. 

Ni dhahiri kwa ukubwa wa klabu hizi mbili kongwe na kwa aina ya shughuli walizokuwa nazo kwa wiki nzima kuelekea kilele cha matamasha yao, mashabiki hata walisahau kwamba jana Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani nje kidogo ya jiji la Nairobi, Taifa Stars walikuwa na mechi muhimu ya marudiano kufuzu Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) dhidi ya wenyeji wao Harambee Stars ya Kenya. 

Hata hivyo, kitu muhimu kwa kilele cha matamasha haya mawili ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki. Kwa mara ya kwanza, Tanzania itawakilishwa na timu tatu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Timu mbili ambazo ni Simba na Yanga zinatoka Bara na wawakilishi wa Zanzibar ni KMKM. 

BINGWA tunataka tuamini licha ya shamrashamra iliyogubika nchi nzima kutokana na kishindo cha klabu hizi mbili kongwe, bado hawajasahau wanajukumu la kupeperusha vyema bendera ya taifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Mafanikio ya timu za Tanzania hususan Yanga na Simba kwa miaka mitatu mfululizo imepelekea Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuogeza idadi ya timu shiriki kutoka Bara kwa michuano ya kimataifa ngazi ya klabu. 

Mechi ambazo Yanga na Simba wamecheza wakiwa kambini ikiwemo zile za kilele cha matamasha yao, BINGWA tunaamini imetumika vizuri kujianda na mechi zao za kimataifa ambapo mwishoni mwa wiki hii watashuka viwanja tofauti kuanza kusaka nafasi ya kutinga kwenye makundi. 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -