Wednesday, November 25, 2020

SIMBA, YANGA TUNASUBIRI SOKA LA KUELEWEKA FEB 25

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MACHO na masikio ya wadau wengi wa soka la Tanzania yanasubiri kwa hamu kuona au kusikia kile kitakachotokea kwenye Uwanja wa Taifa wikiendi hii, ambapo miamba ya soka nchini, Simba na Yanga itavaana katika mchezo wa kuwania pointi tatu muhimu zitakazoiwezesha timu mojawapo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.

Ukubwa wa mchezo huo hautakuwa kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu tu, bali ni heshima baina ya timu hizo zenye upinzani wa jadi kwenye soka la Tanzania tangu zamani.

Simba ambao ndio vinara wa ligi kuu wakiwa na pointi 51 na Yanga wanaokamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 49, wataingia dimbani huku kila mmoja akiwa na nia ya kumwangusha mwenzake na kujihakikishia nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Kama ilivyo kawaida ya timu hizi pindi zinapokaribia kukabiliana, iwe kwenye ligi au michuano mingine, zimekuwa na desturi ya kuweka kambi nje ya Jiji la Dar es Salaam ambalo ndio makazi yao ya kila siku.

Uzito wa mchezo huo wa wapinzani wa jadi unazipa haki ya kutoka nje timu hizo ili kuwa na wakati mtulivu wa kufikiria namna ya kupata matokeo mazuri siku ya mchezo husika.

BINGWA tunatambua wazi ukubwa na umuhimu wa mchezo huo, pia tunaheshimu maandalizi ya timu zote mbili, hivyo ni wazi soka mtakalolionesha Februari 25 pale Taifa litakuwa bora kulingana na maandalizi yenu mliyoyafanya.

Tunatambua kuwa desturi hii ya kuweka kambi nje ya makazi ilikuwapo toka klabu zenu zilivyoanzishwa na mara kadhaa tumeshuhudia mkirudi na mrejesho wa kuridhisha uwanjani.

Katika mchezo wenu wa wikiendi hii, BINGWA tuna matumaini ya kuona burudani ya kutosha, upinzani na nidhamu ya kimchezo kutokana na umaarufu wenu ndani na nje ya nchi.

BINGWA tuna uhakika kuwa Afrika Mashariki kwa ujumla itakuwa inawatazama nyie uwanjani, hivyo hamtatuangusha kwani mechi kati ya Simba na Yanga ni moja kati ya mechi tano bora za wapinzani wa jadi barani Afrika.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -