Friday, December 4, 2020

SIMBA, YANGA ZAUNDA KAMATI ZA MASAA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR,

NI presha tu. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya vigogo na matajiri wa Yanga na Simba kuvamia kambi za wachezaji kwa lengo la kuhamasisha ushindi katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Sambamba na kuvamia kambi hizo, kila upande umelazimika kuunda kamati maalumu, kamati ambazo jukumu lake ni kupata ushindi kuanzia kwenye mchezo huo.

Mechi hiyo inaonekana kuwaweka katika presha kubwa vigogo wa timu hizo ambao wamekuwa wakifanya maandalizi ya kila aina ili kuhakikisha wanapata ushindi.

Yanga ambao wameweka kambi Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa klabu hiyo, Paul Malume na vigogo wenzake, alivamia kambi ya wachezaji wao ili kuwapa hamasa ya ushindi dhidi ya watani wao Simba.

Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo, Malume amewataka kutuliza presha kwani ana imani wanaifunga Simba kwa kuwa ni mechi ya kawaida.

“Ni mechi ya kawaida sana kama unavyojua Yanga ni timu kubwa, tumefanya mazoezi kwa ufanisi, kilichobaki ni kumalizia asilimia 50 uwanjani,” alisema Malume.

Alisema katika kipindi hiki kuelekea katika pambano hilo, mengi yatasemwa lakini aliwataka wachezaji hao kutosikiliza maneno, badala yake waelekeze nguvu na akili zao katika mchezo huo.

Kwa upande wa rais wa zamani wa Yanga, Abbas Tarimba, amewataka wachezaji wa timu hiyo kucheza kwa utulivu na kuwafunga Simba ili kulinda heshima.

Tarimba alisema enzi zake wakati anaiongoza Yanga ilikuwa si rahisi kufungwa na Simba katika mchezo wa ligi na mashindano mengine.

“Mimi nasema hii mechi ni muhimu kwa maana Yanga tunataka kutetea ubingwa wetu na ili tushinde, inatupasa kupambana kwa hali na mali hakuna kingine,” alisema Tarimba.

Alisema wana kila sababu ya kuibuka na ushindi ili kuwapa faraja viongozi wa zamani waliowahi kuiongoza klabu hiyo.

“Unapocheza Yanga ukiwa kama mchezaji, heshima kubwa unaipata kwa kuifunga Simba na utaweza kuishi kama mfalme na popote utakapokwenda huwezi kunyimwa msaada,” aliongeza Tarimba.

“Tunataka heshima hakuna kitu kingine, tuwafunge Simba kesho heshima iendelee kuwepo, lakini pia tunataka ubingwa ubaki Jangwani,” alisema.

Katika hatua nyingine, timu hiyo imeunda kamati ya muda kushughulika na pambano hilo, kamati ambayo hata hivyo vigogo hawakutaka kusema imepewa majukumu gani na itadumu kwa muda gani.

“Elewa tu tumeunda kamati, sasa inafanya kazi gani na itakaa muda gani tuachie sisi,” alisema kigogo mwingine wa Yanga.

Wakati vigogo Yanga wakienda katika kambi ya wachezaji wao, matajiri wa Simba walivuka Bahari ya Hindi kwenda Unguja ambako wachezaji wa timu hiyo wameweka kambi ya siku sita kujiandaa na mchezo huo.

Simba nao waliunda kamati maalumu ambayo inaongozwa na Musley Al Rawahi, ikiwa na wadau mbalimbali wa klabu hiyo kwa lengo hilo hilo la kufanikisha ushindi dhidi ya mahasimu wao.

“Kamati imeenda Zanzibar, lakini pia kuna watu wengine wazito ambao wamekwenda na watarudi kesho (leo) pamoja na timu, mipango imekamilika na tunaamini tutashinda,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye hakutaka atajwe jina lake gazetini.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -