Sunday, November 29, 2020

SIMBA YAPIGA HATUA MBILI MBELE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

KOCHA msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, ameuzungumzia usajili wa msimu ujao wa timu hiyo na kusisitiza utakuwa wa kutisha kulingana na matakwa ya benchi lao la ufundi.

Akizungumza na BINGWA, Mayanja alisema katika kipindi hiki ambacho Ligi Kuu Tanzania Bara imebakisha mechi sita kabla ya kumalizika, wamejipanga kuhahakisha wanauchukua ubingwa baada ya kuukosa kwa miaka minne mfululizo.

“Kwanza tuchukue ubingwa. Unajua baada ya Yanga kuteleza katika mechi na Mtibwa, kwa kweli sikufichi wametupa morali kubwa ya kujipanga kuchukua ubingwa. Ni tofauti na kama wangeshinda, wangekaa pale kileleni ungekuwa mziki mkubwa kuwashusha,” alisema Mayanja.

Mayanja alisisitiza kuwa baada ya ligi kumalizika watasajili wachezaji wenye tija kulingana na mahitaji yao.

“Usajili wetu utazingatia zaidi na nafasi yetu tutakayokuwa nayo. Kama tutashiriki michuano ya kimataifa, ni wazi lazima tuvunje benki kwa kushawishi viongozi wasajili watu wa kazi. Hatuwezi kusajili tu ilimradi. Kama unavyojua, michuano ya kimataifa ni tofauti na ligi,” aliongeza Mayanja.

Alisema kwa sasa kikosi chao kina mapungufu kidogo sana lakini katika dirisha kubwa la usajili msimu ujao huenda wakaelekeza nguvu zaidi katika kusajili wachezaji kutoka nje.

Aidha, Mayanja alisema kikosi cha Simba kimejipanga vema msimu huu kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuwataka wachezaji wa timu hiyo kucheza kwa kujituma kuhakikisha wanaandika historia.

Kikosi hicho kwa sasa kinaongoza ligi kikiwa na jumla ya pointi 55 mbele ya Yanga wanaoshika nafasi ya pili kwa pointi 53, huku timu hizo zikiwa zimeshashuka dimbani mara 24 kila moja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -