Friday, December 4, 2020

SIMBA YAREJESHA ‘UCHAWI’ WA MVUA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA SAADA SALIM,

PAMOJA na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha mjini Bukoba jana, lakini kocha wa Simba, Joseph Omog, hakukatisha mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakiendelea kwenye Uwanja wa Taasisi ya Kanisa Katoliki mjini humo, wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Jumapili.

Lakini hali hiyo ya kuendelea kufanya mazoezi kwenye mvua, iliwafanya mashabiki wachache waliokuwa wamejibanza maeneo jirani kudaiwa kwamba hilo si ajabu kwao kwani ‘mvua ndio uchawi wa Wekundu hao wa Msimbazi’.

Simba inataka kuhakikisha inaondoka Kanda ya Ziwa Kagera na pointi zote tisa katika mechi zao tatu watakazocheza huko, wakianzia mchezo wao huo wa Jumapili katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Vinara hao wa ligi kuu, Wekundu wa Msimbazi wenye pointi 55, wakimaliza mechi dhidi ya Kagera mjini Bukoba, watasafiri hadi Mwanza kucheza na Toto Africans na Mbao FC.

Katika mazoezi yaliyoanza saa 4:00 asubuhi, wakati hali ikionekana kuwa sawa, lakini walipokuwa wakiendelea na mazoezi mepesi, mvua bab kubwa ilianza kupiga, ila kocha wao huyo aliwataka kuendelea hivyo hivyo hadi atakapomaliza programu yake.

Moja ya mazoezi waliyokuwa wakiendelea nayo katika programu ya kocha huyo ni kutaka safu yake ya ushambuliaji kuwa makini na kutopoteza nafasi za kufunga ili kuhakikisha wanabeba pointi tatu muhimu kwenye mechi hiyo.

Meneja wa kikosi hicho cha Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’, aliliambia BINGWA kwamba wamefanya mazoezi kwa muda wa saa tatu, ambapo kila idara kwenye kikosi hicho ilipata nafasi ya kung’amua mapungufu yake na kuyafanyia kazi.

“Tunataka pointi tisa katika mechi zote za Kanda ya Ziwa tukianzia na Kagera. Tukipata ushindi kwenye mechi hiyo itatusaidia kufanikisha mipango yetu ya kutaka kunyakua ubingwa msimu huu,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -