Tuesday, November 24, 2020

SIMBA YAWAKOMOA MASHUSHUSHU WA YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HAWA ABDALLAH, ZANZIBAR

PAMBANO la watani wa jadi kwenye soka la Tanzania, limekuwa la kukomoana kwa timu hizo ambazo zote zimeweka kambi zao za maandalizi visiwani Zanzibar.

Wakati Yanga ikiwa Pemba, Simba imeweka kambi yake Unguja huku ikifanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Aaman, lakini kinachotokea mazoezini hapo kinabaki kuwa siri kwa Wanasimba pekee.

Akizungumza na BINGWA, Mkuu wa Msafara wa Simba, Abbasi Suleiman, alisema kwa kuwa wanajua kwamba mashushushu wa Yanga wanawafuatilia, wamekuwa wakifunga milango ya Uwanja wa Aaman na kwamba hakuna hata shabiki anayeingia kutazama mazoezi hayo.

“Tunahitaji utulivu wa hali ya juu, hatutaki mashabiki waje, lakini zaidi ya hapo tunajua kwamba Yanga wana watu hapa, watakuja na visimu vyao ili wapashane habari, hili tumelidhibiti pia hawataambulia kitu,” alisema Abbas.
Alisema hadi jana jioni, programu ya walimu ilikuwa inakwenda vizuri sana na wana uhakika kwamba watapata ushindi dhidi ya watani zao na kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu.
Aidha, alisema makocha wanaendelea na utaratibu wao waliojipangia katika ufanyaji wa mazoezi kwa wachezaji ili kuhakikisha hawapotezi pointi tatu Februari 25 dhidi ya timu ya Yanga.
“Unajua mechi hii ni ngumu sana, japo si kwamba ndiyo itakayoamua nani anakuwa bingwa msimu huu, lakini inatoa mwelekeo kuelekea kwenye ubingwa, hivyo tunafahamu kila timu inasaka ushindi kwa namna yoyote ile, ndiyo maana tumeona ni bora tujifungie,” alisema.

Simba imetinga kisiwani Unguja Ijumaa ikiwa na wachezaji wote 21 ambao wanaendelea na mazoezi yanayofanyika mara mbili kwa siku; asubuhi na jioni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -