Friday, October 23, 2020

Simba yazidi kuipa kibarua kizito Yanga

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

Lulu Ringo, Dar es salaam

Klabu ya Simba imezidi kuwaumiza kichwa watani wao wa jadi Yanga baada ya jana kuendeleza ubabe kwa kuitungua Ruvu Shooting magoli 5-0 katika uwanja wa Taifa, ushindi uliozidi kuwaweka wekundu wa msimbzi  katika mazingira mazuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Katika michezo miwili mfululizo ikiwa ni ule dhidi ya Alliance na huu wa jana dhidi ya Ruvu Shooting Simba wamejikusanyia jumla ya Alama Sita na magoli 10 tofauti na watani wao.

Katika mtanange uliopita baada ya Simba kumchakaza Alliance goli 5-1, Yanga ilishuka dimbani dhidi ya KMC ikiwa na kumbukumbuku ya ushindi huo, lakini yanga walishindwa kulipa goli hizo baada ya kubanwa mbavu na KMC had walipokuja kupata goli dakika ya 89 kupitia Kiungo wao Feisal Salum (Fei Toto).

Aidha Kesho Yanga itashuka dimbani Kuchuana na wanapaluhengo, Lipuli Fc ikiwa na rekodi mbili za watani wao Simba, rekodi moja ikiwa ni dhidi ya Alliance waliyoshindwa kuilipa kwa KMC na nyingine iliyotengenezwa jana dhidi ya Ruvu Shooting ambapo Simba walishinda tena magoli 5-0 na mchezaji Emanuel Okwi kufunga magoli matatu (hat trick).

Simba Imecheza jumla ya michezo 10 akijikusanyia alama 23 akishika nafasi ya  pili chini ya Azam Fc mwenye alama 27 akiwa amecheza michezo 11 na  Yanga amecheza michezo Nane akiweka kibindoni alama 22 akishika nafasi ya 3 nyuma ya Simba.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -