Tuesday, October 27, 2020

SIMBU: MIALIKO IPO TATIZO WAFADHILI

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA WINFRIDA MTOI


HAKUNA ubishi Tanzania ina safari ndefu katika kuboresha sekta ya michezo na kuifanya iwe moja ya vitu vinavyochangia uchumi wa nchi na kutoa ajira kwa vijana.

Kwenye unafuu kidogo ni katika mchezo wa soka ambapo kwa wale wachezaji waliobahatika kupata nafasi ya kucheza kwenye klabu za Ligi Kuu Bara hususan zile zinazolipa vizuri, wameweza kunufaika na vipaji vyao.

Lakini katika michezo mingine hali bado ni mbaya kwa wanamichezo wake, kwani wengi wanacheza kwa kujitolea wakisubiri zawadi za mashindano endapo mtu atabahatika kufanya vizuri.

Kwa wale waliopata nafasi za kuchukuliwa na timu za taasisi mbalimbali kama jeshini, afadhali unafuu upo kwa sababu wanapata huduma zote muhimu kuliko wale wa klabu za mtaani ambazo hata ada ya kushiriki ikiwekwa Sh 50,000 bado ni shida.

Kwa hali hiyo ya kukosa hata ada ya mashindano ya ndani unategemea mchezo gani unaweza kukua, wakati nguzo kuu ya michezo ni wachezaji kupata mashindano yanayoweza kupima viwango vyao.

Matokeo ya haya yote yanakuja kuonekana wakati timu zipoenda kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa, ambapo kila siku kisingizio cha maandalizi kimekuwa kama wimbo lakini hayafanyiwi kazi.

Picha halisi ya hali ya uendeshaji wa michezo hapa nchini umeweza kudhihirika kipindi cha maandalizi ya mashindano ya Olimpiki, ambapo timu nyingi zilishidwa kwenda hata kwenye mashindano ya kufuzu.

Hata wale waliopata nafasi ya kwenda kushiriki mashindano hayo, asilimia kubwa inatokana na juhudi zao binafsi.

Alphonce Felix Simbu, ni mwanariadha wa Tanzania aliyeweza kuipeperusha vyema bendera ya taifa alipofanikiwa kumaliza nafasi ya tano mbio za marathon kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu yaliyofanyika jijini Rio, Brazil.

Anasema kwa sasa anajiandaa na mbio mbalimbali zitakazofanyika mwakani lakini anakutana na changamoto ya kukosa mtu wa kumsapoti, kwa sababu anataka kwenda kuweka kambi mahali ambako atapata wanariadha wengi wanaokimbia mbio ndefu kama Kenya.

“Kuna mialiko mingi nimeipata ya kushiriki mashindano nje ya nchi na yanatarajia kuanza Januari mwakani, hivyo ninatakiwa kufanya mazoezi sana pamoja na kampani ya wanariadha wenye viwango vikubwa na  natamani sana kwenda Kenya,” anasema Simbu.

Miongoni mwa mialiko aliyoipata ni London Marathon, Boston Marathon na Mumbai Marathon na hii inatokana na kufanya vizuri kwenye mashindano ya Olimpiki.

Anasema kwa kawaida huwezi ukafanya mazoezi na watu wawili au watatu kwa kuwa mbio za marathon zinahitaji kushirikiana mkiwa watu wenye viwango tofauti na ndiyo sababu anapendelea kwenda Kenya mara nyingi.

Simbu anasema maandalizi ndiyo jambo muhimu kwa mchezaji ili aweze kufanya vizuri na endapo anakosa hayo, inakuwa ni tatizo anapoenda kushiriki mashindano makubwa.

“Ujue maandalizi ndiyo kila kitu kwa mwanaridha ili aweze kufanya vizuri, nakumbuka hata kipindi tunajiandaa na Olimpiki mwaka huu, tulipoingia kambini hatukupewa vifaa badala yake tulitumia vya kwetu ambavyo havikuweza kukidhi mahitaji yote,” alisema Simbu.

Anashauri viongozi wa riadha wachangamke kutafuta wadhamini, kwa sababu wanakiri kuwa chama hakina fedha hivyo wanatakiwa kutafuta fursa za kupata fedha kusaidia wanariadha kupata huduma muhimu wanapokuwa kambini.

Simbu anasema kuna vijana wengi wanaojitahidi kutoka nje kwenda kushiriki mashindano tofauti ya kuinua viwango vyao, lakini ushirikiano unahitajika zaidi ili kuweza kufika mbali.

“Kinachotakiwa ni kuhamasisha riadha mikoani kwa kuwa mikoa mingine inashindwa hata kushiriki mashindano ya taifa kwa kukosa hamasa,” anasema.

Aidha, Simbu anasema kuna haja ya kuanza maandalizi ya Olimpiki ya mwaka 2020 kipindi hiki kwa sababu maandalizi yanayozaa matunda ni yale ya muda mrefu.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -