Monday, January 18, 2021

Simeone anaposhindwa kuelewa atakapokuwa miaka 10 ijayo

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MADRID, Hispania

JAPO inashangaza lakini bado kuna watu ambao wanafuatilia kwa ukaribu maisha ya Diego Simione akiwa kama kocha wa Atletico Madrid, ingawa Muargentina huyo naye hajui atakuwa wapi baadaye ndani ya miaka 10 ijayo.

Kocha huyo mwenye hulka ya ucheshi, alisikika akisema hayo kwenye tangazo la kampuni ya magari ya Hyundai akiwa sambamba na mchekeshaji Joaquin Reyes aliyeigiza kama mtangazaji.

Kocha huyo alisikika akilitambulisha gari hilo kabla ya kujibu maswali mfululizo kuhusu maisha yake na alikiri kuwa hana hata wazo ni wapi atakapokuwa mwaka 2026.

“Siwazi mbali hivyo, najichukulia kama mtu anayejaribu kufanya jambo fulani na kufurahia kila siku anayoiishi, siwezi kuwaza wapi nitakapokuwa au nitakuwaje miaka 10 ijayo,” alielezea.

“Mimi ni mtu yule yule kila siku ninayependa utulivu kwenye kasi, hakuna aliyekamilika, hakuna. Lakini watu walio wema huendelea kuwa hivyo,” aliongeza.

Moja ya kanuni iliyokuwa ikimsaidia Sir Alex Ferguson ni namna alivyoweza kusoma alama za nyakati katika soka na Simione pia anaamini hivyo.

“Naamini kwamba ili ujiandae na maisha mazuri ya baadaye inabidi ujiboreshe sasa, baadaye kutajitokeza mambo mapya na inabidi tujiandae lakini wakati huo huo usidharau wakati ulionao. Inabidi uwe mbunifu, hiyo ndio changamoto tuliyonayo,” alisema bosi huyo wa Atletico.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -