Tuesday, December 1, 2020

SIMU NI SUMU AU SUKARI YA PENZI?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

KARIBUNI ndugu wasomaji katika safu hii ya uhusiano wa kimapenzi ambayo huwa inawajia kila Jumamosi na Jumanne, ikitoa nafasi kwenu kufahamu na kuchangia mambo mbalimbali yahusianayo na mapenzi.

Awali ya yote, nitoe shukrani zangu za dhati kwa wote ambao walichangia mada zilizopita.

Baada ya salamu hizo nigeukie mada ya leo ambayo ni matokeo ya maombi ya wasomaji ambao wameomba niirudie kutokana na jinsi ilivyowagusa wengi.

Mada hiyo ilikuwa ikielezea jinsi simu zinavyovunja mahusiano ya wapendanao.

Ndugu msomaji, simu zimekuwa ni moja ya njia rahisi ya mawasiliano baina ya mtu na mtu, japo wakati mwingine, wapo ambao wamekuwa wakizitumia vibaya na mwisho wa siku kuwa sumu ndani ya wawili waliopendana.

Lakini ili simu igeuke kuwa sumu, itategemea na mhusika anavyoitumia, hasa anapokuwa na mwenza wake.

Katika uhusiano wa kimapenzi baina ya wawili wapendanao, kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara inayosababishwa na simu.

Kutokana na hali hiyo, wapo ambao mwisho wa siku wameamua kutozigusa simu za wapenzi wao ili kuepusha shari baina yao.

Wapo ambao hali hiyo imekuwa ni ya kawaida, huku kila mmoja akikubaliana nayo, lakini wengine imekuwa ikiwaumiza mno.

Unapowauliza wale ambao wanakubaliana na hali hiyo, huwa wanadai kuwa kupokea au hata kuchunguza simu ya mpenzi wako ni ushamba na si ustaarabu.

Pia wapo wanaodai kuwa tabia ya kupokea au kuchunguza simu ya mpenzi wako inatokana na wivu wa kijinga na pia tabia hiyo inaonyesha jinsi mtu asivyomwamini mpenzi wake.

Lakini hebu kila mmoja wetu ajiulize, iwapo unampenda kwa dhati mpenzi wako, utajisikiaje iwapo ukiigusa simu yake akakurukia na kukunyang’anya?

Au je, utajisikia vipi iwapo mpenzi wako anapokwenda bafuni anabeba simu yake au anaizima na kuifunga na baada ya kutoka huko ndiyo anaiwasha kama anavyofanya usiku wakati wa kulala?

Lakini je, utajisikiaje pale unapokuwa na mpenzi wako, simu yake ikiita tu, anaizima au kutoka nje fasta kwenda kuipokea huko?

Hebu nitoe fursa kwa wasomaji wa safu hii kuchangia mada hii juu ya suala zima la iwapo ni ulimbukeni au ushamba kuigusa au kuchunguza simu ya mpenzi wako unayempenda kwa dhati ambaye upo tayari kumwona akipotea kwa kudang’anywa na matapeli wa mapenzi ambao kila siku ya Mungu wamekuwa wakibuni mbinu za kuwalaghai wapenzi wa wenzao.

Tukutane Jumanne ya wiki ijayo. Asanteni sana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -