MANCHESTER, England
KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba, amenaswa akiendesha gari huku akizungumza kwa simu yake ya mkononi na huenda akakumbana na adhabu ya kisheria.
Mfaransa huyo alinaswa akiwa anazungumza kwa simu huku akiwa anagonga kinywaji ambacho hata hivyo hakikutajwa kuwa ni pombe.
Kocha Jose Mourinho aliamua kumpumzisha Pogba katika kikosi kilichoisambaratisha Wigan mabao 4-0 katika mchezo wa Kombe la FA.
Pogba ambaye ndiye mchezaji ghali duniani baada ya uhamisho wake kugharimu pauni milioni 89, atarejea ‘mzigoni’ kesho kucheza na Hull City.