Tuesday, October 27, 2020

Simu za Ngassa hazikauki Jangwani

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

LICHA ya Mrisho Ngassa kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Fanja ya Oman, inadaiwa simu za winga huyo hazikauki kwa viongozi wa timu yake ya zamani ya Yanga, akiwa na nia ya dhati ya kutaka kurudi Jangwani wakati wa usajili wa dirisha dogo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba, Yanga, Azam FC na Simba za Dar es Salaam, alitua kwenye kikosi cha wawakilishi hao wa Oman kwenye Ligi ya Mabingwa ya Asia, akitokea klabu ya Free State mwezi uliopita, baada ya kuomba kuvunja mkataba.

Akizungumza na BINGWA, mmoja wa kigogo wa Wana-Jangwani hao alisema Ngassa yupo Oman lakini akili yake ipo Jangwani, huku akiwa na matumaini makubwa ya kuvaa tena uzi wa Wana-Jangwani hao.

“Jamaa ana hamu sana ya kurudi Yanga, lakini tatizo moja ambalo amekutana nalo ni deni la milioni 30 ambalo alikopa benki, huku akidhaminiwa na mwenyekiti, lakini mwisho wa siku akamzunguka akawa anachukua mshahara wake dirishani bila kupitia benki na kukatwa,” alisema  kigogo huyo.

Kigogo huyo alisema ili Ngassa aweze kurejea tena Yanga, hana budi kumwangukia mwenyekiti huyo na kulipa deni hilo, vinginevyo asahau kuichezea tena timu hiyo.
Ngassa alijiunga na Free State Stars Mei mwaka jana, akisajiliwa na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri, kwa mkataba wa miaka minne, lakini bahati mbaya kwake ni kuwa kocha aliyemsajili alitimuliwa kabla hata Ngassa hajacheza mechi za kutosha.

Lakini, baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Free State, Ngassa aliamua kuvunja mkataba na timu hiyo na kutimkia Oman.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -