Thursday, December 3, 2020

SINGIDA UNITED MSIISHIE KWA HANS PLUIJM

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA OSCAR OSCAR

KUFANYA vizuri kwa timu si suala la kuwa na kocha bora peke yake. Unahitaji kila kitu kuwa bora, kuanzia kocha, uongozi mpaka wachezaji, mtihani ambao bado timu iliyopanda daraja, Singida United, wanapaswa kuutazama kwa mapana na marefu.

Wiki iliyomalizika zimetoka taarifa rasmi za klabu ya Singida United kumsainisha aliyekuwa kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm. Ndiyo, Hans ni kocha katika kipindi alichofundisha soka nchini Tanzania, ukiachilia mbali mataji wawili ya Ligi Kuu na lile la TFF, aliifanya pia Yanga kucheza mpira wa kuvutia zaidi.

Lakini yote haya hayakufanikiwa kwa sababu tu Pluijm ni kocha mzuri, Hans alikutana na uongozi mzuri wa Yussuph Manji, alikuwa pia na wachezaji bora kikosini. Wakiwamo kina Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Thaban Kamusoko na mafundi wengine kibao. Yanga ni timu yenye mashabiki kila kona ya Tanzania. Popote unapokwenda mashabiki wake wako nyuma, kuna tofauti kubwa sana ya kuifundisha Singida United na Yanga.

Ni mwanzo mzuri kumpata Hans, lakini Singida United bado haijakamilika. Kama kweli wanataka kuupata ubora wa Hans, wasisite kupiga hodi tena mitaa ya Jangwani. Kumekuwa na utamaduni duniani kote wa makocha kuhama na wachezaji wao wa zamani, na hili linaweza kuisaidia Stand United.

Haruna Niyonzima, Donald Ngoma na Vincent Bossou mikataba yao itamalizika mwishoni mwa msimu huu pale Jangwani. Ni aina ya wachezaji waliofanikiwa wakiwa na Kocha Hans. Hawa ndio aina ya watu wanaoweza kuleta mapinduzi ndani ya Singida na hawa pia wanajua kumtumikia Babu, Hans van der Pluijm.

Huwezi kuishia kusajili kocha bora tu bila kumpatia pia wachezaji bora. Uzuri wa Tanzania, kuna timu tatu tu ambazo kila msimu unapoanza hushindania ubingwa, huku nyingine zote zikikwepa janga la kushuka daraja. Viongozi na wapenzi wa soka mkoani Singida wanapaswa kuchagua uelekeo wao mapema, kama ni kushuka daraja au kuusaka ubingwa.

Miongoni mwa watu waliomfanya Hans Pluijm ajenge kikosi bora cha Yanga ni aliyekuwa katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Dk Jonas Tiboroha. Kuna haja ya Singida United kumvuta kundini Tiboroha. Moja ya watu wanaojua mipango ya soka la kisasa. Bado naamini leo mpaka kesho, Yanga wangekuwa na Tiboroha wasingeyumba kiasi hiki.

Alipata kuwa mshauri mzuri sana kwa Hans Pluijm na naamini bado anaweza kuwa chaguo sahihi kwa timu changa kama Singida United kuanza kuijengea misingi. Wasiishie tu kwenye usajili wa Pluijm, waongeze rasilimali watu wa kumfanya awe imara.

Mataji mawili aliyotwaa ya Ligi Kuu akiwa na Yanga, kuipeleka timu mpaka kwenye hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika, bila shaka inatosha kumwelezea Hans kama kocha mshindani. Wasiwasi wangu haupo kwenye uwezo wa kocha, ni kwenye mazingira yatakayomzunguka kocha huyo wa Kidachi. Atapata wachezaji bora? Timu itatuzwa vizuri? Uongozi utamsaidia kuipa mafanikio timu yao? Haya ni maswali ambayo kwa sasa ni vigumu kuyapatia majibu, lakini muda utaamua.

Mara nyingi timu inapopanda daraja kwa mara ya kwanza, lengo lake mama huwa ni kuhakikisha inabakia Ligi Kuu kwa msimu mwingine zaidi kabla ya kuanza kuuwaza ubingwa na mafanikio mengine. Ni uelekeo mzuri kwa kumsainisha mkataba kocha kama Hans, lakini Singida United wasiishie kwa kocha tu.

Wanapaswa kuwa na uongozi thabiti na wachezaji wenye viwango vya Pluijm. Kuwa na kocha bora peke yake hakutainusuru Singida United. Kuna tofauti kubwa sana ya namna wachezaji wa Simba, Yanga na Azam FC wanavyohudumiwa ukilinganisha na wa klabu nyingine.

Kuna tofauti kubwa mno ya huduma wanazopata makocha wa Klabu kubwa hapa nchini na wale wengine, ni lazima Singida United wampe Pluijm mazingira yanayofanana na alikotoka ili afikie malengo yao. Vinginevyo, tunaweza kushuhudia Babu akishusha heshima yake kwa kutimuliwa asubuhi tu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -