Thursday, October 29, 2020

Siri ya Hazard kung’ara muulize Conte

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

KATIKA siku za hivi karibuni, staa Eden Hazard amekuwa siri ya mafanikio ya Chelsea.

Ikumbukwe kuwa, kwa mara ya mwisho Hazard alikuwa kwenye ubora huu alionao sasa katika msimu wa 2014-15.

Wachambuzi wa soka wanaamini kuwa, kama nyota huyo ataendelea kuwa fiti, basi atakuwa msaada mkubwa kwa kocha Antonio Conte.

Hii ni mara ya kwanza kwa Conte kufanya kazi Ligi Kuu England na ameonesha nia ya kupigania taji la ligi hiyo maarufu duniani.

Msimu uliopita, baada ya kuwachapa Arsenal pale Emirates, kilichofuata ni mikosi kwa Chelesa ambayo kipindi hicho ilikuwa chini ya Mholanzi Guus Hiddink.

Hiddink alishindwa kuipa uhai Chelsea kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Jose Mourinho, ambaye aliishia kutimuliwa.

Kwa sasa, ni kama Conte ‘ameifufua’ Chelsea na Hazard amekuwa roho ya kikosi hicho tangu kuanza kwa msimu huu wa 2016-17.

Mwishoni wa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, mbali na kufunga, Hazard alikuwa kwenye ubora wake wakati Chelsea ilipochomoza na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Manchester United.

Kiwango kizuri cha Hazard msimu huu kimetokana na mabadiliko ya kimfumo aliyokuja nayo Muitalia Conte.

Mfumo mpya wa Conte wa 3-4-3 unamfanya Hazard kuwa huru na kucheza nafasi aliyoitaka kwa kipindi kirefu.

Tofauti na msimu iliopita ambapo alikuwa akirudi kuimarisha ulinzi, sasa Hazard anacheza namba 10.

“Sihisi kuwa na presha, nahisi kuwa na mzuka na najaribu kufanya makubwa zaidi kwa sababu (soka) ndiyo kazi yangu.”

Ukiitazama Chelsea ya sasa, kitendo cha Marcos Alonso kucheza kama winga wa kulia katika safu ya kiungo yenye wachezaji wanne, kimesaidia timu kuwa na uwiano mzuri.

Lakini pia, kwa Conte kuwaruhusu wachezaji wake kucheza kwenye nafasi wanazohisi wanakuwa huru, imesaidia kuamsha ufanisi ambao ulipotea kwa kipindi kirefu.

Hilo linaweza kushuhudiwa zaidi kwa Hazard mwenyewe ambaye kwa kipindi kirefu alitamani kucheza kama mshambuliaji wa kati badala ya winga.

Mkali huyo amepachika mabao mawili katika michezo mitatu tangu Conte alipofanya mabadiliko.

Inaonekana wazi kuwa Conte ametibu ugonjwa uliomsumbua Hazard msimu uliopita na nyota huyo ameanza kulipa fadhila.

Licha ya kumsapoti Diego Costa katika safu ya ushambuliaji, Hazard amekuwa akisababisha madhara makubwa kuliko hata fowadi huyo wa kimataifa wa Hispania.

“Hii ndiyo nafasi yangu,” alisema Hazard.

“Sichezi pembeni katika mfumo huu (3-4-3) na najaribu kupachika mabao,” alidai Hazard.

Ukiachana na mfumo, imeelezwa kuwa Conte alimpa Hazard darasa zito kuhusu kile alichokitaka kwa nyota huyo.

Conte alimjia juu Hazard akimtaka kuweka mbali ustaa wake na kuiweka akili yake uwanjani.

Inadaiwa kuwa, Conte alimchana live staa wake huyo akimwambia hatakiwi kucheza akiwa mabega juu na badala yake ahakikishe anafanya mambo kila atakapopewa nafasi ya kuingia uwanjani.

Kwa darasa hilo, ni wazi Hazard ameelewa na sasa ameielekeza akili yake katika kumjibu kwa vitendo kocha huyo ambaye amewahi kuinoa klabu ya Juventus na timu ya Taifa ya Italia.

Kabla ya kuwatandika Man United, Hazard aling’ara walipoiua Leicester mabao 3-0.

Kwa sasa Conte amemfanya Hazard kuwa tishio zaidi pale mbele, hasa kutokana na kasi yake katika kupandisha mashambulizi.

Kwenye orodha ya wapachikaji mabao, Hazard amepasia nyavu mara nne, idadi ambayo alikuwa nayo kwa msimu mzima wa 2015-16.

Hata hivyo, ikumbukwe kuwa Hazard amekuwa akisumbuliwa na wimbi la majeraha.

Wachambuzi wa soka wanaamini kuwa, tatizo la majeruhi, hasa msimu uliopita lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na nafasi ya winga aliyokuwa akicheza.

Kwa upande mwingine, Hazard si beki, hivyo mara nyingi aliigharinmu Chelsea kila alipocheza nafasi hiyo msimu uliopita.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -