Wednesday, November 25, 2020

SIRI YA KIPIGO SIMBA HII HAPA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY

WAKATI mashabiki wa Simba wakitupia lawama benchi la ufundi la timu yao baada ya kufungwa na Azam bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha wa muda wa Azam, Idd Cheche, amesema tatizo kubwa linaloimaliza klabu hiyo ni papara ya washambuliaji wao wakiwa ndani ya 18.

Bao la dakika ya 70 la mshambuliaji, John Bocco, katika mchezo wa juzi Jumamosi, iliifanya Simba kupoteza mchezo wa pili dhidi ya Azam, baada ya ule wa fainali ya Kombe la Mapinduzi wiki mbili zilizopita.

Akizungumza na BINGWA baada ya mchezo wao kumalizika, Cheche alisema washambuliaji wa Simba wanakuwa na papara kubwa wanapokuwa langoni kwa wapinzani wao, jambo linalosababisha kukosa mabao ya kizembe.

“Ukiangalia katika mchezo wa leo (juzi), Simba wangeweza kutufunga tangu kipindi cha kwanza, lakini walipoteza nafasi nyingi za wazi. Kipindi cha pili hali ilikuwa hivyo hivyo, hata baada ya kuingia kwa Laudit Mavugo, Ibrahimu Ajibu na Shiza Kichuya walionekana kucheza vizuri lakini bado papara iliwamaliza.

“Kama Simba wanataka kupata matokeo mazuri, basi washambuliaji wao wanapaswa kubadilika na kuwa makini, lakini bila ya hivyo wanaweza kufungwa hata na timu ya daraja la pili kwa sababu ya papara ya washambuliaji wao na kushindwa kujiongeza na kuwa makini,” alisema  Cheche.

Wakati huo huo, nahodha wa kikosi cha Azam, Bocco, ameliambia BINGWA kwamba utulivu na kutokata tamaa ndio kilichowasaidia kuondoka uwanjani na pointi zote tatu.

Bocco anaongoza kwa mabao katika mechi kati ya Azam na Simba, ambapo bao lake la jana limemfanya awe ametupia jumla ya mabao saba, akifuatiwa na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo ya Msimbazi, Emanuel Okwi aliyefunga mabao matano.

“Kila mechi nawekewa ulinzi mkali, lakini kitu kikubwa sikati tamaa na kujituma kutafuta nafasi ya kufunga kwa kuwa hilo ndilo jukumu langu kama mshambuliaji,” alisema.

“Hata ukiangalia mechi ya leo (juzi), mabeki wa Simba walifanya kazi nzuri ya kutubana, ila bahati nzuri likatokea kosa nikalitumia,” aliongeza mchezaji huyo ambaye kwa sasa analingana kwa mabao na Amissi Tambwe, Simon Msuva; wote wa Yanga  na Shiza Kichuya wa Simba wote wakiwa na mabao tisa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -