Friday, December 4, 2020

SIRI YA ‘MAUAJI’ YA BARCA KWA PSG

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

CATALUNYA, Hispania

YALIKUWA ni maajabu kwa Barcelona kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya PSG. Haikuwa rahisi kutabiri matokeo hayo kabla ya mchezo.

Kabla ya mchezo huo wa marudiano uliochzewa Camp Nou, tayari PSG walikuwa mbele kwa mabao 4-0, ushindi walioupata katika mchezo wa awali uliochezwa jijini Paris, Ufaransa.

Wakati ulimwengu wa soka ukiamini safari ya Barca kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliishia Ufaransa, wakali hao wakaibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 na kutinga hatua ya robo fainali.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa, siri kubwa ya ushindi huo ni kitendo cha kocha Luis Enrique kutumia mfumo wa 3-4-3.

Kabla ya mfumo huo, tayari mastaa Lionel Messi, Luis Suarez, na Neymar walianza kuonekana kushindwa kung’ara katika michezo mbalimbali.

Lakini pia, hata safu ya kiungo ya Barca haikuwa kwenye ubora wake wa miaka kadhaa iliyopita.

Tangu Enrique aanze kutumia mfumo huo mpya wa 3-4-3, Barca ni kama imezaliwa upya kwenye ulimwengu wa soka.

Ni mfumo huo ndio ulioimaliza Atletico Madrid kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Estadio Vicente Calderon. Lakini pia,  Barca haijapoteza michezo yake minne iliyofuata baada ya Atletico.

Baada ya kuwafunga Atletico mabao 2-1, waliichapa Sporting Gijon mabao 6-1 katika mchezo uliofuata.

Lakini pia, Celta Vigo walikumbana na makali ya mfumo huo baada ya kuburuzwa mabao 5-0.

Lakini pia, idadi ya mabao ambayo ilionekana kuanza kupungua kwenye kikosi hicho imeanza kurejea kwa kasi.

Mpaka sasa, mfumo huo umeshawapa mabao 19, huku nyavu zao zikiwa zimetikiswa mara tatu pekee.

Katika hatua nyingine, inasadikika kuwa makali ya Neymar katika siku za hivi karibuni yamekuwa na mchango mkubwa kwa Barca.

Nyota huyo hakuweza kung’ara katika msimu wake wa kwanza Catalunya, lakini sasa ameanza kuthibitisha ubora wake kikosini.

Takwimu zinaonyesha kuwa, nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ameshafunga mabao manne na kutoa ‘asisti’ mbili katika mechi tatu pekee za hivi karibuni.

Wakati wa ‘mauaji’ ya PSG pale Catalunya, Neymar alipasia nyavu mara mbili na alikuwa mwiba mkali kwa walinzi wa timu hiyo kwa dakika zote 90.

“Ni mchezo bora ambao sijawahi kucheza. Tulijiamini na tukacheza, ni ngumu kuizuia Barca.

“Hii huwa inatokea mara moja katika maisha. Hakuna aliyetarajia kuona tukishinda mabao lakini tulifanya hivyo,” alisema staa huyo wa zamani wa Santos.

Barca wanasubiri fainali yao ya michuano ya Copa del Rey huku wakiwa wameshajihakikishia nafasi robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini pia, kikosi hicho kinaongoza kwenye mbio za kulifukuzia taji la Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -