Tuesday, November 24, 2020

SIRI YA MKUDE YANGA HII HAPA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR


IMEBAINIKA kuwa kitendo cha kiungo wa Simba, Jonas Mkude kuwatosa Yanga katika kipindi cha usajili msimu wa 2014, kimesababisha viongozi wa timu hiyo ya Jangwani kumfungia vioo kiungo huyo ambaye hivi sasa yuko tayari kuichezea timu hiyo.

Mkude, mwenye uwezo wa kumiliki mpira na kufanya kazi ya kuwalinda mabeki wake, huku pia akifanya kazi ya kupanga mashambulizi, mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Vigogo wa Yanga walimweka Mkude kwenye orodha yao baada ya kubaini kwamba mkataba wake unaelekea ukingoni na viongozi wa Simba hawajakaa kujadili ili kumwongezea mwingine kutokana na hali ilivyo ndani ya timu kwa sasa.

Unajua picha kamili likoje? Msimu wa 2014, Yanga walitamani huduma ya kiungo huyo mkabaji wa Simba na wakawa wako tayari kutoa kitita cha Sh milioni 80 ambazo alizitaka na mazungumzo yalifanyika baina ya pande zote mbili na kufikia mwafaka, lakini kinyume na matarajio ya wengi, Mkude aliamua kuwazimia simu Yanga na kusaini Simba.

Wiki iliyopita Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alisema hivi sasa timu hiyo haina mpango wa kumsajili Mkude, hiyo ikiwa ni baada ya kumpata kiungo wa Zesco ya Zambia, Justin Zulu, ambaye tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo.

“Hatuna sababu ya kumsajili Mkude kwa kuwa timu yetu ilihitaji kiungo mwenye uwezo wa kucheza michuano ya kimataifa na si ligi tu peke yake, kimsingi hilo tumefanikiwa baada ya kumpata Zulu,” alisema Sanga.

Naye kigogo mwingine wa klabu hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini aliye karibu na Mwenyekiti wa Yanga, alisema Mkude aliwasumbua sana kupata saini yake katika msimu wa 2014 hivyo hawana sababu ya kumsajili tena katika kipindi hiki.

“Alichezea bahati mwenyewe, kwa Yanga ilivyo hivi sasa pale unafikiri Mkude atacheza sehemu gani? Tuna Kamusoko, Said Juma ‘Makapu’, Justine Zulu, tumekamilika hatutaki tena kupotezeana muda, tunaangalia mbele zaidi katika kipindi hiki,” alisema kigogo huyo.

Iwapo Mkude atatua Yanga huenda akapata wakati mgumu kupata namba kwani timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani ina viungo wengine wengi akiwemo Kamusoko, Makapu, Haruna Niyonzima na Zulu. 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -