Friday, November 27, 2020

SIRI YA ULIMWENGU KUTIMKA TP MAZEMBE HADHARANI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

IMEBAINIKA kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga AFC Eskilstuna ya Sweden, Thomas Ulimwengu, alilazimika kuihama TP Mazembe ya DRC baada ya klabu hiyo kuvunja ghafla mkataba wake.

Inadaiwa Mazembe ilifikia uamuzi wa kuvunja mkataba wa Ulimwengu baada ya mchezaji huyo kupata majeraha yaliyotishia kumweka nje kwa kipindi kirefu.

Uongozi wa Mazembe unadaiwa kumfanyizia Ulimwengu wakati klabu yao ikijiandaa na fainali za Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.

Chanzo cha habari kutoka DRC kimeliambia BINGWA kuwa uamuzi huo usio wa kiuungwana wa kuvunja mkataba wa Ulimwengu, ulienda sambamba na kumlipa stahiki zake zote na kumtaka aondoke mara moja katika klabu hiyo.

“Yaani unajua jamaa wale ni watu wabaya sana, Ulimwengu alikuwa bado ana mkataba na Mazembe lakini kulitokea figisu figisu za ghafla na jamaa wakaamua kukatisha mkataba wake na kumlipa stahiki zake zote, yaani hawakujali mazuri yote aliyowafanyia,” alisema mtoa habari wetu.

Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa kitendo hicho kilimweka katika wakati mgumu mshambuliaji huyo ambaye kipindi hicho alikuwa akisumbuliwa na majeraha.

“Unajua jamaa walijua hataweza tena kupona na kucheza ndio maana wakafanya maamuzi magumu,” kiliongeza chanzo hicho.

Hata hivyo, Ulimwengu kwa upande wake hakuweza kupatikana ili kuzungumzia madai hayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -