Sunday, January 17, 2021

SIRI YA WACHINA KUTEKA ULIMWENGU WA SOKA HII HAPA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

BEIJING, China

WIKI iliyopita timu ya Shanghai SIPG ilikubali kuilipa Chelsea pauni milioni 58 kumchukua Oscar, baada ya  Carlos Tevez kuamua kuiaga klabu yake  kipenzi ya Boca Juniors na kwenda kujiunga na timu ya Shanghai Shenhua kwa ajili ya kuicheza kuanzia msimu ujao.

Katika makubaliano hayo, Oscar atakuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi kutokana na kuwa atakuwa akilipwa pauni 400,000 kwa wiki na klabu hiyo ya jijini Shanghai.

Hata hivyo, Tevez ndiye aliyeingia mkataba mnono ambao atakuwa akilipwa pauni 615,000 akiwa amewazidi mastaa,  Lionel Messi na Cristiano Ronaldo,  katika orodha ya wanasoka wanaokinga mpunga mrefu duniani.

Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni hivi karibuni kuwapo na zilizodai kuwa straika,  Zlatan Ibrahimovic, alikataa mshahara wa pauni milioni moja kwa wiki kwenda China ili aweze kumaliza msimu mwingine akiitumikia  Manchester United, ingawa hakuna shaka atakwenda pindi atakapoamua kuondoka kwenye klabu hiyo ya Old Trafford.

Mbali na huyo, pia mchezaji mwenzake Man United, Wayne Rooney,  ameshatangaziwa ofa ya pauni milioni 75 na klabu hiyo ya Shanghai SIPG, ili aweze kuitumikia kwa muda wa miaka mitatu na huku nyota wa Manchester City, Yaya Toure, naye akiwa ameshakataa kitita cha pauni 577,000 kwa wiki kutoka kwenye klabu ya  Jiangsu Suning, ili aweze kuendelea kukipiga kwenye klabu hiyo ya Ligi Kuu England walau kwa kipindi kingine.

Pia mbali na hao waliochomoa, lakini kuna wachezaji wengine ambao wameshasajiliwa na klabu za nchini humo kwa bei kubwa.

Miongoni mwao ni Givanildo Vieira de Sousa maarufu kwa jina la Hulk ambaye alisajiliwa kutoka klabu ya Zenit St Petersburg na kwenda kujiunga na timu ya Shanghai SIPG kwa ada ya pauni milioni 48, Alex Teixeira, aliyesajiliwa kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk,  kwenda Jiangsu Suning, kwa ada ya pauni milioni 42, Jackson Martinez, kutoka Atletico Madrid kwenda  Guangzhou Evergrande, kwa ada ya pauni milioni 31.

Kutokana na usajili huo wa bei mbaya kumekuwa kumezua maswali mengi ni kwanini Ligi ya China imeanza kwa kasi kuwa suluhisho la wachezaji kuamua kwenda kucheza soka katika nchi hiyo ya Mashariki ya Mbali na ni wapi timu za ligi hiyo zinakopata fedha za kuonesha jeuri hiyo?

Siri ni hii hapa 

Rais wa China, Xi Jinping, ana mkakati mkali kuhusu soka la nchi yake ambao unataka kuleta mageuzi katika ligi ya nchi hiyo maarufu kama Chines Super League.

Katika mpango huo, Rais Xi ameandaa mpango wa miaka 10 ambao ulianzia mwaka 2015 na utakwenda hadi mwaka  2025, ambao utaongeza mara mbili uchumi wa michezo nchini humo kwa zaidi ya pauni bilioni 600 zitakazoelekezwa katika sekta za Serikali na uwekezaji binafsi katika soka.

Kupitia mpango huo, kiongozi huyo anataka kuzalisha wachezaji wapatao  100,000 kwa kuwekeza fedha katika soka la chini na kuanzisha shule mpya za soka zupatazo 20,000 na kujenga viwanja  70,000 ifikapo mwaka 2020.

Mbali na hilo kupitia mpango huo, Rais Xi anataka kuifanya China kuwa moja ya nchi tishio katika michezo na kuiwezesha kufuzu kuandaa fainali za Kombe la Dunia na ikiwezekana kulitwaa

Kwa sasa China inashika nafasi ya 83 katika msimamo wa viwango wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ikiwa katikati ya nchi za Antigua & Barbuda na visiwa vya Faroe na imewahi kushiriki mara moja katika fainali za Kombe la Dunia kabla ya kutupwa nje ya michuano ya kufuzu fainali hizo hatua ya makundi bila kufunga bao hata moja.

Kinachosababisha kutolewa ofa kubwa

 Hadi sasa ofa kubwa zimeshatolewa kwa wachezaji nyota kutoka Ulaya na Amerika Kusini kutokana na kwamba timu za Ligi ya China zina uwekezaji mkubwa.

Mfano timu za Shanghai SIPG, Shanghai Shenhua, Jiangsu Suning na   Guangzhou Evergrande Taobao, ambazo ni mabingwa miaka sita iliyopita ndizo zimekuwa zikimwaga mpunga mnono kusajili wachezaji wenye majina makubwa.

Mbali na hilo pia China imekuwa ikijaribu kulitangaza soka lake nje ya nchi ambao mwaka jana Rais Xi  alidhamini ziara ya timu mpya ya vijana ya Manchester City ukiwa muda mfupi baada ya vyombo vya habari nchini humo kutangaza kuwa Serikali imewekeza pauni milioni 265 katika kampuni hiyo ya Sheikh Mansour na huku timu za West Brom  na  Aston Villa  nazo zikiwa zimepata msaada kama huo.

Mbali pia na hilo mahudhurio uwanjani katika michuano hiyo ya ligi ya China yanatarajiwa kuongezeka katika kipindi cha miaka mitano ijayo na itaweza kupata udhamini mpya wa pauni milioni 935 kutoka vituo vya televisheni na vyombo vingine vya habari.

Utajiri wa baadhi ya wamiliki wa klabu

1.Guangzhou Evergrande, moja kati ya klabu zilizopata mafanikio katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, inamilikiwa na Kampuni ya Evergrande Group (60%), ambayo ni moja ya kampuni kubwa za ujenzi nchini humo na Kampuni ya Alibaba (40%).

2.Jiangsu Suning, inamilikiwa na Kampuni ya  Suning Commerce Group, ambayo ni moja ya kampuni kubwa za biashara.

2.Beijing Guoan, mwanahisa mkubwa ni Kampuni ya CITIC Group ambayo inamilikiwa Serikali.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -