Thursday, October 29, 2020

Sita waweka ngumu Yanga, Ngasa safii

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

UONGOZI wa Yanga chini ya Mwenyekiti wake, Dk. Mshindo Msolla, umeingia katika presha kubwa baada ya wachezaji wao sita wa wakutegemewa kutokuwa na uhakika wa kuendelea nao msimu ujao.

Yanga ni miongoni mwa timu ambazo wachezaji wao wengi wa kikosi cha kwanza wanamaliza mikataba, huku kukiwa na taarifa kuwa kuna baadhi yao wameshaanza mazungumzo na klabu nyingine.

Taarifa ambazo BINGWA limezipata kutoka ndani ya Yanga kwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Ufundi inayosimamia masuala ya usajili, zinasema kuwa kikosi chao kina wachezaji 10 wanaomaliza mikataba yao.

Imeelezwa kuwa kati yao, Yanga imepanga kuwaongezea mikataba wanne tu ambao ndio waliohitaji kiasi kikubwa cha fedha.

Wachezaji wanaomaliza mikataba yao mwisho wa msimu huu ambao Yanga inahitaji kuendelea nao ni Mohamed Issa ‘Mo Banka’, Jaffar Mohammed, Deus Kaseke, Said Juma Makapu, Papy Tshishimbi na Juma Abdul, huku Mrisho Ngasa akiwa kwenye makubaliano maalumu na uongozi, hivyo ataendelea kuwapo Jangwani.

“Wachezaji baadhi wameshakaa mezani na uongozi kuzungumzia mkataba, mfano ni Tshishimbi ambaye amehitaji milioni 80 badala ya  60 ambayo GSM wametaka kumpa, lakini pia yupo Banka, Jaffar na Makapu, hao wamehitaji milioni 65 kila mmoja wakati uongozi ulipanga kuwaongezea dau na kufika 50, huku Kaseke akihitaji mara mbili zaidi ya ile aliyopewa awali.

“Uchunguzi tulioufanya baada ya kuona kila mchezaji anaweka ugumu katika kuongeza mkataba, tumebaini tayari kuna timu zimefanya mazungumzo nao ambazo ni Azam FC, Polisi Tanzania na Simba, hivyo ndio maana wameweka ugumu wakitaka tufike pale walipohitaji wao,” alisema.

Mjumbe huyo aliongeza: “Hali hiyo inaiweka Yanga katika wakati mgumu kwani wanaweza kuwapa kile wanachohitaji, lakini tayari wamefanya mazungumzo na timu nyingine, hivyo tunahofia huenda wakaja kushawishiwa kuihujumu timu huko mbele kama ambavyo imewahi kutokea kwa baadhi ya wachezaji wetu msimu huu.”

Mbali ya nyota hao, wachezaji wengine ambao mikataba yao imefika ukingoni jana baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kufika ukingoni, ni David Molinga, Ngassa, Rafael Daudi, Andrew Vincent ‘Dante’ na Kelvin Yondani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -