Saturday, January 16, 2021

SITARAJII KUONA WAAMUZI WAKIVURUNDA VPL 2017/18

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAINAB IDDY

MBIO za kuufukuzia ubingwa wa msimu wa 2017/19 wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), zinatarajia kuanza leo kwa  viwanja saba kuwaka moto nchini.

Msimu huu unatazamiwa kuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki wa soka kutokana na timu 16 zitakazoshiriki kufanya maandalizi mazuri.

Kumekuwa na tambo nyingi hasa katika kipindi cha dirisha la usajili, ambapo kila timu imejinasibu kufanya makubwa ili kuwafurahisa mashabiki wake.

Katika msimu huu, kutakuwa na timu tatu mpya, ambazo ni Lipuli ‘Wanapaluhengo’ ya Iringa, Njombe Mji kutoka mkoani Njombe pamoja na Singida United ‘Watoto wa Mwigulu’,  ambayo ipo chini ya kocha  mzoefu  Hans van der Pluijm ambaye ni kocha mwenye rekodi nzuri tangu alipokuwa Yanga.

Lakini sasa kuelekea msimu mpya, kilio cha muda mrefu kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu pamoja na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Daraja la Pili (SDL) ni kuvurunda kwa waamuzi.

Ni wazi huu umekuwa ni wimbo wa kila unapokaribia msimu mpya. Imekuwa ni kawaida kwa klabu zinazoshiriki ligi hizo kueleza kusikitishwa kwake na ubovu wa waamuzi.

Kwa miaka mingi, jambo hilo limekuwa likiondoa ladha ya soka, mchezo unaopendwa zaidi duniani kote.

Umekuwa ni utamaduni katika soka la Tanzania kushuhudia waamuzi wakifungiwa kila msimu kutokana na kushindwa kuzitafsiri vyema sheria 17  za soka.

Uzembe huo umekuwa ukiibua hasira kwa mashabiki na kujikuta wakianzisha vurugu na kufanya uharibifu mkubwa viwanjani ikiwamo kung’oa viti kama ilivyowahi kutokea katika moja ya mechi za mahasimu Simba na Yanga.

Ikumbukwe kuwa msimu uliopita ulitawaliwa na matukio mengi ya waamuzi kufungiwa kutokana na matukio yao ya kushindwa kuzitendea haki sheria za soka.

Mfano mzuri ni mwamuzi mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Martin Saanya, ambaye aliondolewa katika orodha ya kuchezesha michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kushindwa kumudu pambano dhidi ya watani wa jadi Simba na Yanga, uliochezwa Oktoba mosi mwaka jana.

Saanya alishindwa kwenda na kasi ya pambano hilo lililokuwa na presha kubwa, ambalo pia huvuta hisia za mashabiki wengi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

Mwamuzi huyo alijikuta kwenye matatizo kwa kitendo chake cha kutoa kimakosa adhabu ya kadi nyekundu kwa nahodha wa Simba, Jonas Mkude na kisha kulikubali bao lenye utata la mshambuliaji, Amissi Tambwe, aliyetajwa kuunawa mpira kabla ya kuutumbukiza wavuni.

Mwingine aliyekumbana na adhabu ya kufungiwa kutokana na kushindwa kutafsiri vyema sheria ni Rajab Mrope, mwamuzi aliyechezesha mchezo uliozikutanisha Yanga na Mbeya City.

Mrope aliingia kwenye majanga hayo kwa kitendo chake cha kuchelewa kutoa uamuzi baada ya bao lililofungwa na nahodha wa Mbeya City, Kenny Ali, ambaye alipiga mpira kabla ya kuruhusiwa na mwamuzi huyo.

Ilishangaza zaidi pale Mrope alipolikataa bao hilo na baadaye kulikubali baada ya kuzongwa na wachezaji wa Mbeya City.

Wakati hayo yakijiri, kubwa zaidi  lilikuwa ni lile la utata wa kadi za mchezaji, Mohamed Fakhi, ambapo mwamuzi alishindwa kuwa na rekodi ya kadi alizotoa katika michezo aliyochezesha.

Hilo lilisababisha utata mkubwa na kusababisha mashabiki wa soka kutokuwa na imani na waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu Bara.

Ni sakata hilo ndilo lililosababisha uongozi wa klabu ya Simba kugomea kupokea zawadi ya mshindi wa pili,  ukidai kufanyiwa hujuma na waamuzi.

Viongozi wake walipeleka malalamiko yao Fifa ambapo hadi sasa hawajajibiwa.

Kwa wadau wa soka wanaoota maendeleo ya mchezo huo hapa nchini, wasingetarajia kuyaona makosa hayo yakijirudia msimu huu.

Bila shaka Chama cha Waamuzi (FRAT) na Bodi ya Ligi wamejipanga vema kuhakikisha mapungufu hayo hayapati nafasi msimu huu wa 2017/18.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -