Saturday, November 28, 2020

SOLLY MAHLANGU WA AFRIKA KUSINI KUWASILI LEO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

MWANAMUZIKI wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini, Sorry Mahlangu, anatarajiwa kuwasili leo akitokea nchini Afrika Kusini kushiriki Tamasha la Kimataifa la Injili la Pasaka litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo ambaye pia ni mchungaji, anatarajia kuwasili nchini leo kuendelea na maandalizi mengine kabla ya kufanyika kwa tamasha hilo kubwa hapa nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, alisema kamati yake inaendelea na maandalizi kuelekea tamasha hilo ambalo litashirikisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.

Msama alisema kuelekea katika Tamasha hilo Makamu wa Rais Samia Suluhu amekubali kuwa mgeni rasmi lakini atawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba.

“Makamu wa Rais amekubali kuwa mgeni rasmi siku hiyo, lakini atawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, kwani siku hiyo Makamu wa Rais atakuwa nje hivyo kuwakilishwa na Mwigulu.

Alisema wasanii hao watatumbuiza siku hiyo ya tamasha na kuwataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kushuhudia tamasha hilo kwenye Uwanja wa Taifa.

Alisema mbali na wasanii hao kutumbuiza siku hiyo, pia kutakuwa na dua maalumu ya kumwombea Rais Dk. John Magufuli.

Mbali na kumwombea Rais Magufuli, pia wataitumia siku hiyo kuwatunuku tuzo viongozi wa Serikali waliofanya vyema katika vipindi vyao vya uongozi.

Msama alisema pia siku hiyo ya tukio watazindua albamu ya msanii Rose Muhando, Kwaya ya Livaifu ya Kinondoni.

“Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Iringa, Simiyu, na Dodoma wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama.

Msama alisema baadhi ya waimbaji wengine waliothibitisha kushiriki  tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Jesca Honore, Christina Shusho na Kwaya ya Unyankulu kutoka Tabora.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -