Thursday, December 3, 2020

SOUTHAMPTON WATAIVURUGA MAN UNITED FAINALI YA EFL?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

FAINALI ya mwaka huu ya Kombe la Ligi (EFL Cup) kati ya Manchester United na Southampton itakuwa ni ya 50 kufanyika katika Uwanja wa Wembley na mashabiki wamekuwa wakishuhudia mabao mazuri na maajabu makubwa.

Moja ya kituko cha kwanza kilikuwa mwaka 1967 wakati timu ya Daraja la Tatu, Queens Park Rangers walipoichapa timu ya Ligi Kuu West Bromwich Albion na tangu hapo maajabu yameendelea, ambapo Obafemi Martin, alifunga bao la ushindi dhidi ya Arsenal.

Ushindi wa historia wa Luton mwaka 1988 na John Sheridan, aliibania timu yake ya utotoni Manchester United mwaka 1991.

Je, itakuwaje fainali ya mwaka huu? Southampton wataivuruga Manchester United na kunyakua taji hilo?

Kikosi hicho cha Jose Mourinho, Man United waliichapa Northampton Town katika raundi ya tatu kabla ya kutinga robo fainali kwa kuichapa Manchester City 1-0, kisha wakatoa dozi ya 4-1 kwa West Ham.

Nusu fainali yao dhidi ya Hull City haikuwa rahisi, hasa kutokana na klabu hiyo ya Tigers, kubadilika kutokana na ujio wa Marco Silva, wakishinda mechi ya kwanza 2-1 na United kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mechi zote mbili.

Kwa upande wa Southampton, walikuwa na kazi ngumu ya kuichapa Crystal Palace, Sunderland, Arsenal na Liverpool na kutinga fainali.

United watakuwa wanasaka taji lao la tano la Kombe la Ligi, wakati kocha wa Saints, Claude Puel, atakuwa akiwania taji lake la kwanza tangu atue St Mary’s akirithi mikoba ya Ronald Koeman, aliyejiunga na Everton mwaka jana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -