Wednesday, October 28, 2020

Staa anapozoea kufanya jukumu lenye madhara baadaye

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

CATALUNYA, Hispania

WIKIENDI iliyopita, mshambuliaji mahiri wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi, aliipatia timu yake hiyo ushindi mtamu ugenini wa mabao 3-2 dhidi ya Valencia, kwa kufunga penalti katika dakika ya 94 ya mchezo huo uliopigwa dimba la Mestalla.

Ushindi huo ulikuwa na maana kubwa katika harakati zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Hispania, pia kwa Messi mwenyewe kwenye suala zima la rekodi yake ya ufungaji mabao katika maisha yake ya kusakata kandanda.

Kwa miaka yote hiyo, Messi anatambulika kama mwanasoka aliyebarikiwa mno duniani.

Ni mkokotaji mzuri wa mpira, anatengeneza nafasi na kufunga mabao, lakini rekodi yake ya kufunga mabao kwa penalti hairidhishi, ambapo katika penalti zake zote alizowahi kupiga, staa huyo ameshindwa kufunga asilimia 20 ya penalti hizo.

Ni mtu anayeaminiwa kupiga penalti ndani ya Barca na mara chache katika miaka ya hivi karibuni, ameonekana kumwachia Neymar apige lakini pale mambo yanapoonekana kuwa magumu, yeye mwenyewe huchukua jukumu zito.

Kwa kawaida Messi si mtu wa kukubali kushindwa kufanya, lakini msimu uliopita alishindwa kufunga penalti nne kati ya nane, ikiwa ni takwimu mbovu kwake hadi kupelekea wadau wengi kudhani ufundi wake unapungua.

Penalti huwa hazitabiriki, hili linajulikana lakini kwa wachezaji wenye uwezo mzuri wa kushughulika na eneo hili wanajulikana.

Messi alifunga penalti hiyo dhidi ya mlinda mlango mwenye rekodi nzuri ya kudaka penalti katika historia ya La Liga. Ni bao alilofunga kutokana na presha ya mchezo husika na imetabiriwa kwamba, kwa takribani muongo mmoja ujao (iwapo ataendelea kuichezea Barca), rekodi yake haitavuka kiwango katika sekta ya kupiga penalti licha ya kuwa ndio mtu muhimu hapo.

Kwanini mastaa wa timu ndio huchukua jukumu hilo? Katika miaka ya hivi karibuni, yule mpigaji mzuri wa penalti kwenye timu hapigi, bali yule staa ndiye mwenye jukumu, jambo ambalo halikuwepo hapo kabla.

Inahisiwa kwamba labda mastaa hawalaumiwi pindi wanapokosa penalti, ndiyo maana wamekuwa wakiaminiwa sana.

Mfano mzuri ni mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero. Huyu tayari ameshindwa kufunga penalti nne msimu huu kwa timu yake ya taifa na klabu, lakini bado anaendelea kuchukua jukumu hilo kila inapopatikana.

Si kwamba kuna wachezaji ambao hawafurahii kuchukua jukumu hilo, lakini Aguero ataendelea kuwa mpigaji penalti chaguo la kwanza la City.

Kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola, ni aina ya mwalimu ambaye anawataka wachezaji wake wachague wenyewe nani atafanya kitu fulani na nani afanye kipi uwanjani na hawawezi kumwangusha Aguero katika hilo, kwani kuna mfano mwingine wa mpigaji mzuri wa penalti, Kelechi Iheanacho, lakini kwa pamoja wamekubaliana nani achukue jukumu.

Tukirudi katika miaka ya nyuma, takribani miongo miwili au mitatu, mabeki ndio waliozoeleka kupiga penalti.

Penalti za Arsenal zilipigwa na beki wa kushoto, Nigel Winterburn, pale Man United pia beki wa kushoto, Denis Irwin, (kabla ya hapo zilikuwa zikipigwa na beki wa kulia).

Kiungo wa zamani wa Liverpool, Jan Molby, alifunga mabao nane ya Ligi Kuu England, licha ya kwamba hakufunga bao lolote nje ya penalti hizo kwa wakati huo, lakini hilo halikuwa jambo la ajabu kwani alijulikana kuwa ni mpigaji maalumu wa penalty, huku straika Ian Rush akiwa wa pili.

Kwa mashabiki wa Liverpool, watakumbuka umahiri wa Rush katika kupachika mabao, hivyo kama angekuwa anacheza soka la kisasa, basi wangempa jukumu la kupiga penalti zote za timu.

Huo ni upande wa penalti, vipi kuhusu faulo?

Staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ameshuka kiwango cha kupiga mipira ya namna hiyo kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Alipokuwa kwenye ubora wake pale Man United na miaka yake ya awali ndani ya Madrid, Ronaldo aliweza kufunga kuanzia asilimia nane hadi 10 katika ‘frikiki’ zake.

Lakini msimu wa 2014-15, uwiano wake wa kupiga frikiki ulishuka hadi asilimia sita na hata asilimia nne mwaka uliopita, kwa mujibu wa mtandao wa takwimu wa Opta.

Si takwimu ya kuridhisha kwani mabao ya aina hii ni ya kipekee na mara nyingi mipira inapogonga mabeki kabla ya kuingia au makosa ya walinda milango, ndio huwa inapelekea takwimu za wapiga ‘frikiki’ kuwa nzuri.

Lakini takwimu hizo nazo zimedhihirisha kuwa zile frikiki za Ronaldo hazina hatari tena kama ilivyokuwa hapo awali.

Lakini kama angekuwa ndani ya klabu nyingine, angekuwa mpiga faulo wao maalumu lakini yupo Madrid, sasa hivi winga mwenzake, Gareth Bale, ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kufanya hivyo.

Kwa wale wanaofuatilia mienendo ya mawinga hao, mashuti ya faulo za Bale yana hatari mno hivi sasa kuliko yale ya Ronaldo ambayo mara nyingi yamekuwa yakipaa juu, kitu ambacho ni nadra mno kwa staa huyo aliyekuwa akitegemewa mno katika sekta hiyo.

Tofauti na miaka ya nyuma pale Santiago Bernabeu miaka ya 2000, ambapo beki wa kushoto, Roberto Carlos, alipiga asilimia kubwa ya faulo mbele ya mafundi wengine kama Zinedine Zidane, Luis Figo na Ronaldo de Lima ambao walikuwa na uwezo wa kufunga mabao katika eneo hilo.

Mpaka alipokuja kutua kiungo, David Beckham, mwaka 2003 Mbrazil Carlos alianza kutumika kwa asilimia chache mno, ingawa mara chache faulo za yadi 35 ambazo zilionekana kuwa ni za mbali mno kwa Beckham.

‘Galacticos’ (mastaa zaidi ndani ya timu) hao wa Madrid walikuwa mfano mzuri sana wa wachezaji ambao huhusika mno katika maamuzi binafsi; kitu kinachotakiwa kuepukika ndani ya timu yoyote.

Kwenye suala la penalti, kila kitu kipo wazi.

Mchezaji anayeonekana kufunga sana mabao ya faulo, hudhaniwa kuwa na uwezo mzuri wa kuendelea kufunga kwa mtiririko mzuri, lakini kwa yule anayekosa penalti mbili au tatu kwa mfululizo, vitu vingi huanza kupungua kwa kuzingatia mafanikio yake na ya timu kwa ujumla.

Messi anaonekana kurudi kwenye kasi yake, kama atarudia fomu yake ambayo haikuridhisha kama alivyorudi majeruhi msimu uliopita, hata mabao yake binafsi hayatakuwa na nguvu kubwa sana ya kuisaidia Barca ishinde mechi zake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -