Wednesday, October 28, 2020

STAA GANI ATAIBEBA TIMU YAKE EPL HADI MEI MWAKA HUU?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England


NI miezi minne imesalia kabla ya Ligi Kuu England kumalizika na kila timu inapambana jino kwa jino kuhakikisha inamaliza kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.

Vita kubwa iliyopo kwa sasa ni kwenye ‘top four’ ambapo timu nne zimepishana kwa tofauti ya pointi moja tu, lakini timu hizo nne zinaungana na nyinginezo mbili ambazo zinakimbia kwa kasi kuhakikisha zinatinga kwenye nafasi hizo nne za juu na kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Je, ni mchezaji gani atakayekuwa muhimu ndani ya kila kikosi cha timu hizo sita hadi ifikapo Mei mwaka huu? Makala hii imechambua kila timu na mchezaji wake muhimu atakayekuwa silaha ya hatari.

 

Chelsea

Tangu msimu huu umeanza mshambuliaji, Diego Costa, ameviteka vyombo vya habari kwa mitazamo chanya na hasi, lakini Eden Hazard, ndiye mchezaji aliyeonesha kiwango cha hali ya juu msimu huu.

Ni wachezaji wachache wanaokipiga Ligi Kuu England wenye uwezo wa kufanya kazi kubwa anayoifanya Mbelgiji huyo mwenye mabao tisa na pasi tatu za mabao msimu huu.

Tangu alipotua kwenye ligi hiyo 2012, ameweza kuwa mmoja wa wachezaji bora wa Chelsea ndani ya misimu minne kati ya mitano aliyoitumikia klabu hiyo hadi sasa.

 

Liverpool

Wakati Philippe Coutinho akionesha uwezo wake wa kushambulia huku Jordan Henderson, akiichezesha vyema timu ya Liverpool katika nafasi yake ya kiungo wa dimba la chini, Roberto Firmino, ni mchezaji bora wa Liverpool pindi timu inapokuwa na mpira na hata inapousaka kuurudisha kwenye himaya yao.

Firmino ni mchezaji mzuri kwa kukaba kuanzia eneo la mpinzani, huisaidia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kuanzisha mashambulizi ya kasi. Pia ni mchezaji bora linapokuja suala la kufanya maamuzi ya haraka na yenye faida pindi Liverpool inapofika kwenye eneo la hatari la mpinzani.

Liverpool imepata faida nyingi msimu huu kwa kumtumia Firmino kama mshambuliaji wa kati, ingawa kwa sasa kasi yake imepungua kutokana na majeruhi ya wachezaji wenzake hivi karibuni.

 

Arsenal

Hakuna ubishi kwa sasa Alexis Sanchez, ni mchezaji hatari zaidi wa Arsenal licha ya kurudishwa pembeni baada ya straika Olivier Giroud kurudi kwenye kiwango chake.

Ubora wa Sanchez umeelemea zaidi kwa jinsi anavyojipanga uwanjani.

Msimu huu amekuwa ni mfungaji mzuri na mzalishaji wa mabao na anao uwezo wa hali ya juu wa kucheza kwenye eneo lolote la ushambuliaji kama ilivyo kwa Hazard.

Sanchez anaweza kupiga mashuti makali, pasi za uhakika, ni mkokotaji mzuri akiwa na mpira, ukimpanga kulia, kushoto, mshambuliaji pekee au nyuma ya straika bado ataifanya kazi yako kwa ufasaha na kwa nguvu zote kadiri awezavyo.

Haitaingia akilini kwa sasa kama Arsenal itakubali kumwachia Mchile huyu kwa dau lolote lile.

 

Tottenham

Mfumo wa kocha, Mauricio Pochettino, unahitaji wachezaji wenye uwezo wa kukaba na kushambulia kwa pamoja na kasi ya hali ya juu.

Wapo wengi wanaofanya vizuri ndani ya kikosi cha Spurs msimu huu, lakini hawafikii kazi kubwa anayoifanya kiungo wa Denmark, Christian Eriksen.

Ubunifu wake pindi Spurs inapokuwa na mpira kwenye himaya yao unamfanya Eriksen kuwa mmoja wa wachezaji bora wa Ligi Kuu England hivi sasa na wakati Dele Alli na Harry Kane, wakifanya kazi nzuri wafikapo langoni mwa mpinzani, Eriksen ameonesha ubora mwingine wa kutambua ni muda gani anaotakiwa kutoka kwenye eneo lake la kiungo cha kati (namba 8) na kufunga mabao pia.

 

Man City

Licha ya kocha Pep Guardiola, kubadili kikosi na mifumo mara kwa mara, bado ana wakati mgumu wa kujua ni timu ipi ya kuichezesha msimu huu.

Sergio Aguero bado anaendeleza umahiri wake linapokuja suala la kufunga mabao, wakati kiungo tegemeo wa ukabaji, Fernandinho, akishindwa kuzuia hisia zake msimu huu na kujikuta akipata kadi nyingi nyekundu.

Ni Kevin De Bruyne, pekee anayefanya kazi nzuri ndani ya mipango yote ya Guardiola ambaye amekuwa akimtumia kama kiungo wa dimba la chini huku akibadilishana nafasi na wenzake akiepuka kukaa kwenye eneo moja muda mrefu.

 

Man United

Baada ya kuanza msimu na kiwango cha chini mno, kiungo wa Man United, Paul Pogba, ameibuka kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi hicho kwa siku za hivi karibuni.

Mourinho kwa sasa ameanza kumtumia kama kiungo huru, kitendo kilichosaidia United kupata matokeo mazuri ya kushinda mfululizo hivi karibuni.

Licha ya kiwango chake dhidi ya Liverpool wikiendi iliyopita kuwa chini, Pogba atakuwa mchezaji muhimu wa United miaka michache ijayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -