Tuesday, October 27, 2020

Stand United yajipanga kutoa mikong’oto tu

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA EZEKIEL TENDWA

BAADA ya kufanikiwa kucheza michezo sita bila kupoteza, benchi la ufundi la Stand United limeibuka na kudai kuwa malengo yao ni kutwaa ubingwa msimu huu bila kupoteza mchezo wowote.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha msaidizi wa Stand United, Athuman Bilal ‘Billo’, alisema kasi waliyoanza nayo haitapungua hata kidogo mpaka ligi inamalizika na kwamba kila timu itakayoingia kichwakichwa kwao haitatoka salama.

“Tunamshukuru Mungu mambo yetu yanakwenda kama tulivyotarajia, tulijipanga tangu mwanzo kuhakikisha msimu huu tunafanya vizuri na ndicho kinachojionyesha.

“Kucheza michezo sita bila kupoteza ni kitu ambacho hakijitokezi mara kwa mara, nadhani soka tunalolionyesha ni zuri na tunachotaka ni kuwa hivi mpaka ligi inamalizika kwani msimu huu tumedhamiria kutopoteza mchezo wowote,” alisema.

Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Mbeya City katikati ya wiki hii, alisema maandalizi yanakwenda vizuri na kwamba watahakikisha wanaibuka na ushindi licha ya kuwa watakuwa uwanja wa ugenini wa Sokoine.

“Muda huu (jana) tunapozungumza tupo njiani tunaelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo, ninaamini utakuwa mchezo mgumu lakini tutapambana hadi tone la mwisho ili kuondoka na pointi,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -