Wednesday, October 28, 2020

‘Stand wasiifananishe Simba na vitu vya kijinga’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA REBECCA LUZUNYA, MWANZA

KOCHA msaidizi wa Simba ya jijini Dar es Salaam, Jackson Mayanja, ni kama ameitaka timu ya Stand United kutoifananisha Simba na vitu vingine baada ya kusema kwamba timu hiyo ya Shinyanga isijisumbue kufikiria ushindi kwenye mchezo wao wa Jumatano kwa kukariri historia ya kuwa eti waliifunga Yanga na Azam.

Mayanja amesema hayo juzi baada ya kumalizika kwa mchezo wake na Mwadui na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, ushindi uliozidi kuwaweka kileleni mwa ligi na kufikisha pointi 32.

Alisema watahakikisha wanapambana zaidi kadiri wawezavyo kuhakikisha wanachukua pointi tatu nyingine kutoka kwa Stand licha ya timu hiyo kuonekana kutoa upinzani mkali kwa timu kubwa msimu huu.

Alisema licha ya timu hiyo kuonekana kukamia ushindi dhidi yao watawatumia vyema wachezaji wao kuhakikisha hawapotezi katika mchezo huo ili kufanikisha malengo yao ya kuondoka na pointi zote Kanda ya Ziwa.

“Kikosi changu kina wachezaji wengi kama mlivyoona leo hatumtegemei mmoja na endapo atapata nafasi akashindwa kuitumia anatoka na kuingia mwingine, kwa hali hiyo hatuna wasiwasi na Stand,” alisema Mayanja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -