Saturday, November 28, 2020

STARS HII TUSITARAJIE JIPYA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

MWANZONI mwa wiki hii, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga, alitangaza kikosi chake cha wachezaji 26 ambao wataisaka tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Mastaa walioitwa Stars ni Aishi Manula (Azam), Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga), Said Mohammed (Mtibwa Sugar), Shomary Kapombe (Azam), Hassan Ramadhani ‘Kessy’ (Yanga), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba), Gadiel Michael (Azam), Andrew Vincent ‘Dante’ (Yanga), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam FC).

Wengine ni Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Said Ndemla (Simba), Frank Domayo (Azam), Muzamil Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (DC Tennerife) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).

Pia, Mayanga amewaita kikosini washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden) na Ibrahim Ajib (Simba).

Mbali na mtihani huo wa kwanza wa Chan, ‘jeshi’ hilo litakuwa na kibarua kingine cha kufukuzia nafasi ya Tanzania kwenye michuano ya Afcon ya mwaka 2019, itakayofanyika nchini Cameroon.

Kabla ya kuingia vitani kuzisaka tiketi hizo, kikosi hicho cha mastaa 26 kitacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Botswana na Burundi.

Baada ya kuingia kambini Machi 19, Stars itashuka Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Machi 25 kucheza na Botswana, kabla ya kuwakaribisha Burundi siku tatu zitakazofuata.

Safari ya Stars katika michuano ya Chan itakayofanyika mwakani nchini Kenya itaanza kati ya Julai 14 na 16, ambapo itamenyana na Rwanda, kabla ya timu hizo kurudiana kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali, kati ya Julai 21 na 23.
Kama itafanikiwa kuwatoa Amavubi, Tanzania itavaana na mshindi kati ya Uganda na Sudan Kusini au Somalia katika raundi ya tatu.

Kwa upande wa Afcon 2019, Stars itaisaka tiketi ya kwenda Cameroon ikiwa Kundi  linalozijumuisha Uganda, Cape Verde na Lesotho.

Mayanga hakuchukua wachezaji wapya wengi, kwa maana kwamba hakutaka kuanza kuijenga timu upya, ikizingatiwa kuwa muda uliobaki kabla ya kuanza kwa mechi za kufuzu ni mchache.

Mastaa ambao hii ni mara yao ya kwanza kuvaa ‘uzi’ wa Stars ni Mbaraka Yussuf anayeichezea Kagera Sugar na Abdulrahman Juma wa Ruvu Shooting.

Nyota hao walipata bahati hiyo baada ya kutemwa kwa majeruhi John Bocco ‘Adebayor’, Abdi Banda na Shomari Kapombe.

Katika hatua nyingine, Mayanga alisema kikosi chake hakitakuwa na wachezaji kutoka Zanzibar kutokana na kusubiri uamuzi wa kikao cha Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuhusu kuipa uanachama rasmi nchi hiyo.

Kama Zanzibar itapewa uanachama wake na CAF, wachezaji wake hawataruhusiwa kuingia Stars, lakini kama ombi lao litakwama wataendelea na majukumu yao ya kuibeba bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Mayanga, kuna nafasi nne alizoziacha kwa wachezaji wa Zanzibar ikiwa Kisiwa hicho hakitafanikiwa katika harakati zake za kutaka uanachama wa CAF.

Lakini habari zilizotangazwa juzi katika vyombo vya habari, zimeeleza kuwa, tayari Zanzibar imepewa uanachama wa CAF katika kikao kilichofanyika mapema siku hiyo, ikiwa ni kutokana na jitihada za Rais wa TFF, Jamal Malinzi, aliyekuwapo katika mkutano wa chombo hicho cha soka Afrika na kusimama kidete kupigania hilo.

Hata hivyo, bado kikosi cha kocha Mayanga na wasaidizi wake wa benchi la ufundi kimeonekana kuwa na mapungufu makubwa, ikizingatiwa kuwa, kina mtihani mkubwa uliopo mbele yake. Inatia shaka kuamini kuwa uteuzi wake utaitoa Stars hapa ilipo.

Hakuna anayeweza kupinga uwezo wa Mayanga hata kwa bahati mbaya, lakini kuna uwezekano mkubwa wa uteuzi wake kumwangusha katika jukumu alilonalo la kuhakikisha Stars inatinga Chan na Afcon 2019.

Uteuzi wake umeonekana kuwa wa kutozingatia takwimu za wachezaji aliowahitaji kwenye safari yake hiyo ambayo mara nyingi imekuwa ikihitimisha vibarua vya makocha wa kigeni.

Unawezaje kuwaita wachezaji ambao wameshindwa kujihakikishia namba kwenye timu wanazotoka? Mfano wa wachezaji kama Hassan Kessy, Erasto Nyoni, Andrew Vincent na Said Ndemla.

Mbali na hilo, hakukuwa na ulazima wa kuwaita wachezaji waliorejea uwanjani katika siku za hivi karibuni baada ya kukaa nje kwa muda mrefu wakiuguza majeraha.

Ukichunguza kilichowafelisha makocha wengi waliopita Stars, utagundua kuwa, walianza kuchemsha katika aina ya wachezaji waliowaita kwenye vikosi vyao. Tofauti na Mayanga ambaye pia uteuzi wake una kasoro tajwa hapo juu, wengi walibeba wachezaji wenye umri mkubwa ambao walishindwa kuendana na kasi ya makinda uwanjani.

Mayanga ni miongoni mwa makocha bora na wenye historia ya mafanikio katika timu alizozinoa, lakini uteuzi wake ni kamari kwake, Stars na soka la Tanzania katika medani ya kimataifa.

Lakini pia, kwa upande wake, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lina kila sababu ya kubeba mzigo wa lawama ikiwa Mayanga atafeli kwenye mipango yake.

Viongozi wa Shirikisho hilo watalazimika kuwa wa kwanza kupokea shutuma ikiwa Stars haitakwenda Kenya au Cameroon kucheza michuano ya Chan na Afcon 2019.

Bado kumekuwa na sintofahamu juu ya nafasi ya kocha mkuu kwenye kikosi cha Stars na inaelezwa kuwa, Mayanga amekalia kiti hicho kwa muda tu.

Taarifa zilizopo zinasema kiti hicho kitakaliwa na Kim Poulsen, ambaye anatarajiwa kusafiri na kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys.

Poulsen atakwenda na Serengeti Boys nchini Gabon ambako ndiko zitakapofanyika fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri huo (Afcon U-17).

Ukichunguza kwa makini, utagundua kuwa kwa kipindi kifupi kilichobakia kabla ya kuanza kwa mechi za kufuzu Chan na Afcon 2019, kuna uwezekano wa Stars kunolewa na makocha wawili.

Tunatarajia nini kutoka kwa timu hiyo, ikizingatiwa kuwa Mayanga na Poulsen ni makocha tofauti na kila mmoja ana falsafa yake? Ni majanga tu.

Wakati wachezaji wakianza kumwelewa Mayanga, ghafla watabadilishiwa mbinu na kocha mpya, Poulsen, ambaye kwa kipindi hicho atakuwa amerejea kwenye kiti chake.

Mikanganyiko ya aina hii, pamoja na uteuzi wa kikosi usiozingatia takwimu za wachezaji, vimekuwa chanzo cha Tanzania kuvurunda katika michuano ya kimataifa kila mwaka.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -