Tuesday, November 24, 2020

STARS INAIHITAJI CHAN SI AFCON

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HASSAN DAUDI

TAIFA Stars inakabiliwa na mtihani wa kukata tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan).

Mbali na hilo, timu hiyo inahitaji kufanya kweli kwenye michezo ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa Afrika (Afcon) za mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.

Hizo ndizo changamoto tatu kubwa ambazo zimeishikilia hatima ya soka la Tanzania kwenye medani ya kimataifa.

Ieleweke kuwa si rahisi kwa Stars kushiriki michuano yote hiyo (Chan na Afcon).

Lazima mipango ya Stars ilenge aidha Chan au Afcon na si kutarajia itafuzu kote.

Kwa bahati mbaya, bado viongozi wenye dhamana ya kusimamia soka hapa nchini hasa wale waliopo TFF, hawajaiweka hadharani dira ya Stars. Wapi nguvu kubwa ya Stars ilipoelekezwa?

Nadhani tulihitaji mwongozo kutoka kwao, ambao ungeweka wazi ‘target’ ya soka la Tanzania katika mashindano hayo mawili ya kimataifa.

Walipaswa kutujibu, Stars inaihitaji Chan itakayofanyika Kenya au Afcon ya Cameroon.

Hata hivyo, kwa kuzingatia hali ya soka la Bongo, Stars inaihitaji zaidi michuano ya Chan kuliko Afcon.

Kwa kuwa Tanzania ina idadi ndogo ya wachezaji wa kulipwa, lazima uimara wa Stars utokane na wengi wanaocheza ligi ya ndani.

Tofauti na nchi zenye mastaa wengi barani Ulaya, soka la Tanzania linapaswa kuanza kuwekewa mizizi kupitia wachezaji wa ndani, hasa wale wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chan ambayo hushirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani, ndio unaopaswa kuwa msingi wa kulijenga jina la Tanzania kwenye ulimwengu wa soka.

Kama Stars itafanya vizuri Chan ikiwa na wachezaji wa ndani, hakutokuwa na haja ya kuendelea kulilia uhaba wa mastaa wanaocheza Ulaya na safari ya Afcon na Kombe la Dunia itakuwa nyepesi katika siku za usoni.

Nini kilitokea wakati nyota saba wa timu ya Taifa ya Cameroon ‘Indominatable Lions’ wanaokipiga Ulaya walipokataa kujiunga na kikosi hicho katika fainali za Mataifa Afrika za mwaka huu (2017)?

Alichokifanya kocha wa kikosi hicho, Hugo Broos, ni kutumia idadi kubwa ya wachezaji wa ndani na ndio waliyoipa ubingwa timu hiyo.

Hilo lilitokana na ubora wa wachezaji wao wa ndani. Hilo ni somo zuri kwa Tanzania juu ya umuhimu wa kuwa na kikosi imara kinachoundwa na wachezaji wa ndani.

Hapo ndipo unapokuja umuhimu wa mashindano ya Chan katika kuwajenga wachezaji wanaocheza Ligi Kuu Bara na si kuwategemea Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Farid Mussa, ambao ndio wachezaji pekee wanaocheza Ulaya.

Michuano hiyo itakayofanyika mwakani nchini Kenya ni muhimu kwa Stars kuliko kutarajia miujiza Afcon.

Kwa soka la Bongo ambalo wachezaji wake wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi hawafikii watano, ni ngumu kuamini itafuzu au kufanya vizuri kwenye michuano ya Afcon au Kombe la Dunia nchini Urusi.

Ni mapema mno kuamini Stars ya kocha Mayanga ina uwezo wa kuzitoa jasho Cameroon, Senegal, Ivory Coast au Ghana.

Wakati Tanzania ikiwa na wachezaji watatu pekee tegemeo wanaocheza Ulaya, Samatta, Ulimwengu na Farid, mataifa hayo yana utitiri wa ‘maproo’ wanaotawala kwenye ligi kubwa barani humo.

Lakini pia, hata Misri ambao mara nyingi wamekuwa wakitegemea wachezaji wanaocheza ndani, bado Stars itahitaji maombi ya kutosha kuifikia.

Mfumo wa soka uliopo Misri ukiwamo uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye shule za kukuza na kulea vipaji ‘academy’, hauwezi kuufananisha na huu wa hapa nchini.

Pia, Waarabu hao wamewekeza zaidi katika mifumo ya kisasa ya uendeshaji soka, hakuna ‘figisufigisu’ katika masilahi ya mchezo huo.

Kwa mantiki hiyo, ni wazi kuwa ni ndoto kutarajia makubwa kutoka kwa Stars ikiwa nguvu kubwa itawekezwa kwenye michuano ya Afcon.

 

Mipango ya kuifufua Stars ambayo haijacheza Afcon tangu mwaka 1980, inapaswa kuanzia kwa wachezaji wa ndani, yaani kuitumia ipasavyo michuano ya Chan.

Huenda kufanya vizuri kwa Stars katika mashindano hayo ya mwakani kukawavuta mawakala wa kimataifa kuangalia vipaji vya wachezaji wa ndani. Lakini pia, Chan ni njia nyepesi ya kuitangaza Ligi Kuu Tanzania Bara.

Maendeleo ya mchezo wa soka katika nchi zilizopiga hatua huwa na misingi yake na huwa hayaibuki kimaajabu.

Kwa maana hiyo, Stars isikwepe ngazi za mafanikio, ianze na Chan, halafu Afcon na Kombe la Dunia vitafuata.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -