Wednesday, November 25, 2020

STARS MSIMWACHE VIBAYA NAPE NNAUYE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo inatarajiwa kuivaa Botswana katika mchezo wa kirafiki ikiwa ni siku chache tangu kuondolewa kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Nape ameondolewa na Rais John Magufuli na nafasi yake kuzibwa na Dk. Harrison Mwakyembe ambaye atashuhudia mchezo wa leo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, iwe ni kwa kufika uwanjani au kutazama kwenye luninga.

Kuondoka kwa Nape haikuwa habari nzuri kwa wanahabari, kwani wengi wao walionekana kuvutiwa na utendaji kazi wake kwa mwaka mmoja aliokuwapo madarakani.

Lakini Nape pia alikuwa mhimili mkubwa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambapo alikuwa akisapoti timu za taifa hasa Taifa Stars kuhakikisha inafanya vema kwenye michezo yake.

Hakuna asiyejua kuwa Nape alikuwa akijitolea kwa hali na mali kuhakikisha timu hizo zinafanya vema kwenye michezo yake yote.
Hivyo, Taifa Stars chini ya Salum Mayanga, inapaswa kumuaga kwa heshima kiongozi huyo kwa kuhakikisha ushindi kwenye mchezo wao wa leo.

Tunajua wachezaji wako tayari kutumia kwa jasho lao lote kutokana na mafunzo pamoja na mbinu mbalimbali walizopewa ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

Wachezaji wetu wanatakiwa kuhakikisha wanaifunga Botswana leo ili kuiwezesha Tanzania kupanda katika viwango vya soka vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ikiwa ni baada ya kuporomoka kwa kasi na kifika nafasi ya chini kabisa katika historia ya nchi yetu.

Iwapo Stars itashinda mchezo huo wa kalenda ya FIFA pamoja na kuipandisha Tanzania, lakini pia kitendo hicho kitasaidia kurejesha morali ya Watanzania kwa timu yao hiyo.

Tutake tusikate inaonekana wazi mashabiki wa soka nchini leo watajitokeza Uwanja wa Taifa si kutokana na mapenzi ya timu yao hiyo, lakini ni kuona shujaa wao, Mbwana Samatta anayekipiga katika kikosi cha Genk ya Ubelgiji anafanya nini.

Ikumbukwe kuwa tangu Samatta ameanza cheche zake na kuuwasha moto katika Ligi ya Ubelgiji, zaidi ikiwa ni ile ya Ligi ya Europa, Watanzania hawajapata fursa ya kumwona ‘live’ akifanya yake.

Zaidi ya hayo, tumalizie kwa kuwatakia kila la heri wachezaji wa Stars kuelekea mchezo huo wa leo dhidi ya Botswana, tukiamini vijana wetu wanaweza kufanya kweli na kurejesha matumaini ya Watanzania dhidi ya timu yao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -