Sunday, November 1, 2020

STEPHEN CURRY; MKALI ALIYEUTIA PRESHA UFALME WA LEBRON JAMES NBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA CHARLES FROLIAN (TSJ)

STEPHEN Curry si jina geni kwa mashabiki wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) kutokana na uwezo mkubwa alionao na kuibeba timu yake ya Golden State Warriors hadi kufika fainali za NBA kwa miaka miwili mfululizo.

Jina lake kamili ni Wardell Stephen Curry, mzaliwa wa Akron Ohio, Marekani. Machi 14, 1988 ndiyo tarehe yake ya kuzaliwa akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu.

Curry amekulia kwenye familia ya wanamichezo ambapo baba yake, Dull Curry, aliwahi kuwa kwenye kikosi cha Cleverland Cavaliers cha mwaka 1988, wakati huo akijulikana zaidi kwa jina la Curry 1.

Mzazi wake huyo alikuwa ni shujaa wake, Curry alifuata nyayo zake baada ya mzazi wake huyo kumjengea misingi ya kuupenda na kucheza mchezo huo kwa moyo mmoja.

Mama yake Stephen aitwaye Sonya Curry, ni muumini mzuri wa dini ya Kikristo na anaupenda mchezo wa mpira wa kikapu, mara kadhaa Stephen amekiri kuwa mama yake amekua na mchango mkubwa kwenye mafanikio yake.

“Mama yangu amenifundisha kuwa na hofu ya Mungu na kumtumainia yeye peke yake,” Curry alizungumza maneno hayo alipokamilisha uhamisho wake kutoka kwenye chuo cha Davidson na kutua Warriors.

Ilipofika mwaka 2009, Curry alifanikiwa kuwa mfungaji bora katika mashindano ya mpira wa kikapu kwenye ngazi ya vyuo. Aidha, alifanikiwa kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi NBA kwa miaka miwili mfululizo, 2014-15 na 2015-16 huku akiwashinda wakali kama LeBron James, Kevin Durant, Dwyane Wade, Tim Duncan na wengineo.

Curry amefanikiwa kuvunja rekodi mbalimbali ikiwemo ile ya mitupio ya mbali ya alama tatu huku akifikisha jumla 272 kwa mwaka 2013 na kuivunja rekodi hiyo yeye mwenyewe msimu wa mwaka 2016-17 kwa kufunga jumla ya alama 286.

Kumekuwa na ubishani wa nani zaidi kati ya LeBron James na Curry kutokana na upinzani mkubwa wanaooneshana na hilo linachangiwa na ubora wa timu zao pamoja na kukutana mara kadhaa kwa siku za karibuni.

Wakali hao wamekutana kwenye fainali mbili mfululizo za 2014-15 na 2015-16 na kila mmoja kuibuka mbabe huku wakizisaidia timu zao kuibuka na ubingwa.

Mara ya kwanza kukutana ilikua msimu wa mwaka 2015, Curry akiiongoza timu yake ya Warriors iliyokuwa na wachezaji kama Draymond Green, Klay Thompson, Andre Iguodala na kuichapa bila huruma Cleverland Cavaliers iliyoongozwa na James kwa jumla ya michezo 4-2 na kuchaguliwa kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi kwa mwaka huo (MVP).

Msimu uliofuata wa mwaka 2016 walifanikiwa kukutana tena kwenye mchezo wa fainali, safari hii mshindi akiwa ni James baada ya kukiongoza kikosi chake cha Cavaliers kilichoundwa na wachezaji kama Kyrie Irving, Kevin Love, Richard Jefferson, kuichapa  Warriors iliyoongozwa na Curry kwenye mchezo ambao ulivuta hisia za mamilioni ya mashabiki wa mchezo wa kikapu duniani kote.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -