Friday, October 23, 2020

Straika aliyeitoa udenda Yanga atua

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA MARTIN MAZUGWA

MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya soka ya Union Sportive de Douala ya Cameroon, aliyeitoa udenda Yanga Mghana, Awudu Zakari, ametua nchini akiisaka timu ya kujiunga nayo katika usajili wa dirisha dogo huku akimtaja kocha wa Simba, Joseph Omog, kama mmoja wa makocha anaotamani sana kufanya nao kazi.

Akizungumza na BINGWA jana alipotembelea ofisi za gazeti hili, Zakari alisema amekuja nchini kufanya kazi lakini anavutiwa zaidi kufanya kazi na Omog kutokana na rekodi za kocha huyo wa zamani wa timu ya vijana ya Cameroon.

“Namjua Omog siku nyingi tangu akiwa anafundisha timu ya vijana ya Cameroon, aliwafundisha nyota wengi ambao nilikuwa nacheza nao huko, ni moja ya makocha bora ambao mimi ningetamani sana kufanya nao kazi,” alisema.

Alisema pia anaijua klabu ya Simba kupitia kwa rafiki yake Mganda, Hamis Kiiza ambaye walicheza pamoja nchini Misri katika klabu ya Nogoom el Mustaqabal inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri, Kiiza alicheza msimu mmoja klabuni hapo kabla ya kuondoka na kujiunga na Free State ya Afrika Kusini.

Zakari alisema hii ni mara ya kwanza kwake kuja hapa nchini lakini pia anaijua klabu ya Yanga ambayo imeshakuwa na wachezaji kadhaa wa Ghana, lakini pia kutokana na kufundishwa na Hans van der Pluijm ambaye ni kocha mwenye rekodi nzuri sana nchini Ghana.

Mchezaji huyo alikutana na Yanga ilipokwenda nchini Ghana katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama, lakini Yanga walishindwa kumsajili kutokana na kujaza nafasi za wachezaji wa kimataifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -