Sunday, November 1, 2020

Straika Toto African aibua tuhuma nzito

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI,

MSHAMBULIAJI wa Toto African, Waziri Junior amesema mchawi mkubwa wa timu yao ni kukosekana kwa ushirikiano miongoni mwa wachezaji wa kikosi hicho.

Akizungumza na BINGWA jana, Junior alisema kikosi chao kimekuwa kikishindwa kutengeneza nafasi hatua inayosababisha kukosa ushindi katika mechi mbalimbali za ligi kuu msimu huu.

Alisema yeye binafsi anaamini bado anao uwezo mkubwa wa kupachika mabao isipokuwa kinachosababisha ashindwe kung’ara ni kuwepo kwa ubinafsi baina ya wachezaji wa timu hiyo.

Junior aliitaja sababu nyingine iliyoifanya timu hiyo kusuasua msimu huu ni mabadiliko ya makocha ya mara kwa mara ingawa alidai athari zake si kubwa sana kama ya ubinafsi miongoni mwa wachezaji.

“Kuna mabadiliko makubwa kati ya kikosi cha msimu uliopita na huu wa sasa, kwa sababu wachezaji hatuna ushirikiano uwanjani, kocha amekuwa akituelekeza juu ya jambo hilo lakini tukija uwanjani kila mtu anafanya yake,” alisema Junior.

Toto inakamata mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi nane baada ya kushuka dimbani mara 12, ikishinda mbili, sare mbili na kupoteza mara nane.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -