Monday, October 26, 2020

STRAIKA YANGA MARUFUKU MADEMU DAR

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HUSSEIN OMAR

STRAIKA wa Yanga, Emmanuel Martin, ameanza kuwapa kitu roho inapenda mashabiki wa timu hiyo, baada ya kuonyesha vitu muhimu na adimu katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kutokana na  kiwango alichokionyesha katika mechi mbili za mzunguko wa  pili wa Ligi Kuu Bara, ni wazi kwamba Yanga hawakufanya makosa ya kumsajili.

Straika huyo alisajiliwa katika dirisha dogo la Ligi Kuu Bara akitokea JKU ya Zanzibar, baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina, kuridhishwa na uwezo wake.

Lwandamina hakuchelewa kumvuta kwenye kikosi chake na kumsainisha mkataba, baada ya  kuwafunga mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Baada ya kuwavutia pia mashabiki wa timu hiyo, straika huyo sasa ametahadharisha kutojihusisha zaidi na mapenzi na anasa za dunia ili asishushe kiwango chake.

Akizungumza na BINGWA juzi, baadhi ya mashabiki hao walisema pamoja na kuridhishwa na uwezo wa straika huyo, lakini ana wasiwasi wa yeye kupoteza namba iwapo atazama kwenye anasa za dunia.

Mmoja wa wanachama wa Yanga  kutoka Tawi la Magomeni, jijini Dar es Salaam,  Ibrahimu Mussa, alisema ili aendelee kufanya vizuri anatakiwa kuachana kabisa na anasa za dunia.

Alisema baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu hiyo, alianza vizuri na kuona wamepata mchezaji lakini walipoanza anasa viwango vyao vilionekana kushuka.

Alisema wachezaji wengi wa Kitanzania wameshindwa kulinda viwango vyao kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha huku wakipenda starehe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -