Monday, January 18, 2021

STUMAI ABDALLAH ‘KUCHINARDO’; Binti mwenye kipaji cha ajabu cha soka

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MARTIN MAZUGWA

LIGI Kuu ya Soka ya Wanawake ilianza Novemba Mosi, mwaka huu, katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo baadhi ya timu zilionyeshana kazi kuona ni vipi zinaweza kushinda michezo yao ya awali tayari kupigania ubingwa wa kwanza kabisa wa kipute hicho.

BINGWA lilibahatika kuhudhuria moja ya mechi za ligi hiyo kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ambapo JKT Queens ilikuwa ikicheza na Mlandizi Sisters.

Mara tu baada ya kuanza kwa mchezo huo, kuna binti ambaye alikuwa akitupiwa mno macho na mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo kutokana na vitu adimu alivyokuwa akivionyesha, zaidi ikiwa ni katika kumiliki mpira, kupiga chenga na kufunga mabao.

Baada ya mchezo huo ulioishia kwa JKT kushinda mabao 4-1, BINGWA lilimfuata binti huyo ambaye anafahamika kwa jina la Stumai Abdallah. kama ilivyojionyesha katika orodha ya majina ya wachezaji na kufanya naye mahojiano.

BINGWA: Hongera sana kwa kiwango ulichokionesha leo na kufanikiwa kufunga mabao mawili.

STUMAI: Ahsante sana.

BINGWA: Unaweza kutupa historia yako kwa ufupi katika soka?

STUMAI: Nimezaliwa Agosti 25, 1997 na nilianza kucheza soka nilipojiunga na Shule ya Sekondari ya Makongo mwaka 2011 hadi 2014, nilipohitimu kidato cha nne, niliendelea na soka.

BINGWA: Kabla ya hapo hukuwa umewahi kucheza soka?

Stumai: Nilianza kucheza soka nikiwa na umri wa miaka 12, nilipokuwa darasa la saba mkoani Ruvuma nilikozaliwa.

BINGWA: Nini kilikuvutia hadi ukaingia katika soka?

STUMAI: Niliamua kuingia katika mchezo wa soka kwa kuwa nilijiona kuwa naweza kucheza, ndiyo sababu nikaamua kujiingiza katika mchezo huu, nilianza kuupenda tangu nikiwa mdogo, nilikuwa nikijiapiza kuwa siku moja lazima na mimi nicheze soka.

BINGWA: Namba gani unaimudu zaidi kucheza uwanjani?

STUMAI: Mimi ni kiraka, nacheza namba zaidi ya moja uwanjani, hivyo  inafuatana na maamuzi ya kocha atakavyoamua kunipanga, katika mchezo husika nacheza beki ya kati, kiungo na ushambuliaji, nafasi ambayo siwezi ni kusimama langoni (kipa).

BINGWA: Wewe ni shabiki wa timu hapa nchini na nje ya nchi?

STUMAI: Hapa nchini naipenda klabu ya Simba toka nilipokuwa mdogo, lakini kwa upande wa  nje ya mipaka ya Tanzania naipenda zaidi klabu ya Manchester United kwa sababu ni moja kati ya timu bora na kongwe  yenye  rekodi nzuri  barani Ulaya .

STUMAI: Unaizungumziaje ligi ya mwaka huu?

Ligi ni ngumu, inahitaji maandalizi ya kutosha ili uweze kufanya vizuri zaidi, ndiyo maana mwalimu wetu amekuwa mkali pindi tunapokuwa mazoezini hataki tufanye masihara.

BINGWA: Mchezaji gani anakuvutia zaidi katika mchezo wa soka?

STUMAI: Hapa nchini hakuna, lakini nje ya mipaka ya Tanzania navutiwa na kiungo nyota wa klabu ya Arsenal, raia wa Ujerumani, Mesut Ozil, ambaye ni mmoja kati ya viungo bora zaidi ulimwenguni.

BINGWA: Nini maana ya jina lako la utani la Kuchinardo?

STUMAI: (Anacheka) ni jina la utani nililopewa na wachezaji wenzangu, wakimaanisha Ronaldo wa Kusini kutokana na kutokea mikoa ya kusini.

BINGWA: Mbali na Ruvuma Queens, ni timu gani nyingine umewahi kuichezea?

STUMAI: Nilipokuwa nasoma Makongo pia nilikuwa nacheza katika kikosi cha Evergreen, ambacho hata msimu uliopita wa ligi nilikuwa nakichezea.

BINGWA: Ni aina gani ya kiatu unachopenda kuvaa ukiwa uwanjani?

STUMAI: Napenda zaidi kuvaa kiatu aina ya Nike, naamini ni kiatu chenye bahati kwangu na kila ninapokivaa nafanya vizuri, hata wachezaji wakubwa pia wanapendelea aina hii ya kiatu, akiwemo mwanasoka bora wa dunia,       Cristiano Ronaldo.

BINGWA: Nini malengo yako ya baadaye?

STUMAI: Mungu akijaalia malengo yangu ni kucheza soka nje ya mipaka ya Tanzania, ndiyo ndoto yangu kubwa kama nitakuwa na uhai.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -